Msafara wa Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa ukipokelewa kwa shangwe na wanaCCM na Wananchi wa Mji wa Babati, Mkoani Manyara, wakati alipowasili kwenye mji huo kusaka wadhamini watakaomuwezesha kutapa ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI.
Sehemu ya Wakazi wa Mji wa Babati wakimshangilia Mh. Lowassa pale walipomuona.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akimsalimia Kijana Jacob Jeremiah ambaye ni mlemavu wa miguu, alipokutana nae nje ya Ofisi Kuu ya CCM Mkoa wa Manyara, iliopo Mjini Babari leo Juni 25, 2015, wakati akiwa katika ziara ya kusaka wadhamini watakaomuwezesha kutapa ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015.
Safari ikiendelea.
Mh. Lowassa akisaini kutabu cha Wageni cha Ofisi ya CCM Wilaya ya Babati, Mkoani Manyara.
Muimbaji wa Nyimbo za Injili, Bahati Bukuku akiimba moja ya nyimbo zake wakati akiwasalimia WanaCCM na Wananchi wa Mji wa Babati, Mkoani Manyara leo Juni 25, 2015.
Sehemu ya WanaCCM na Wananchi wakazi wa Mji wa Babati Mkoani Manyara, wakiwa kwenye Uwanja wa CCM Wilaya ya Babati.
Mjumbe wa NEC kutoka Wilaya ya Mlele, Mkoani Katavi, Kampala Thomas Maganga akiwasalimia wanaCCM wa Mji wa Babati Mkoani Manyara.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Jesca Msambatavangu akisema neno wakati akiwasalimia wanaCCM na Wananchi wa Mji wa Babati, Mkoani Manyara leo Juni 25, 2015.
WanaCCM wa Babati Mkoani Manyara.
Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Mh. Kiseryi Chambiri akizungumza jambo wakati Mh. Lowassa alipofika kuomba udhanini wa WanaCCM wa Mji wa Babati, Mkoani Manyara leo Juni 25, 2015.
Meza kuu.
Tabasamu la Mh. Lowassa baada ya maneno ya Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Mh. Kiseryi Chambiri.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Mh. Edward Lowassa akipeana mkono na Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Mh. Kiseryi Chambiri.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Edward Lowassa akipokea fomu ya udhamini kutoka kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Babati Mjini, Daniel Ole Porokwa, leo Juni 25, 2015. Mh. Lowassa amepata udhamini wa wanaCCM 42, 405 wa Mkoa wa Manyara.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mtangaza nia ya kuwania Urais wa Tanzania, Edward Lowassa akizungumza wakati akiwashukuru wanaCCM wa Mkoa wa Manyara, waliomdhani ili apate ridhaa ya chama chake kuwania Urais wa Tanzania kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, 2015. Lowassa amepata wadhamini 42, 405 , Mjini Babati Mkoani Manyara leo, Juni 25, 2015.
1 comment:
Wot a waste of resources!!
Post a Comment