Mwanamke mwenye umri mdogo pamoja na
mtoto wake wamekutwa wakiwa hai siku tano baada ya ndege waliokuwemo
kuanguka kwenye msitu magharibi mwa Colombia.
Mwanamke huyo Maria Nelly Murillo, 18, na mtoto wake wa mwaka mmoja wamekutwa na
waokoaji karibu na ndege hiyo yao ndogo aina ya Cessna iliyoanguka
kwenye Mkoa wa Choco.
Mkuu wa Kikosi cha Anga cha Kolombia
ameelezea kuwa kunusurika kwa mama huyo na mtoto wake ni muujiza.
Murillo alikuwa na majeruhi na kuungua lakini mtoto wake alikuwa
mzima kabisa.
Mtoto wa mwanamke huyo akiwa amebebwa na muokoaji
No comments:
Post a Comment