ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 26, 2015

Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima AFP, Said Soud Said, Atangaza Nia kugombea Urais 2015

Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima AFP Mhe Said Soud Said, akiwasili katika viwanja vya Idara ya Habari Maelezo Rahaleo kutangaza nia na kulaaani kitendo cha Mawaziri wa kutoka CUF kususia Kikao cha baraza la Wawakilishi Zanzibar, akiongozana na Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa AFP Ndg Shaibu Masoud
Mhe Said Soud Said akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali kuhusiana na kutangaza Nia ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama chake cgha AFP, Na kulani kitendo cha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa CUF Kususia Kikao cha Bajeti wakati wa kuchangia Bajeti ya Wizara ya Fedha Zanzibar.
Mhe Akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika ukumbi wa Habari Maelezo Rahaleo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima ( AFP) Said Soud akizungumza na Waandishi wa Habari hawapopichani akizungumza kulaani kitendo cha Chama cha Wananchi (CUF) kutoka katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi kulia ni Afisa wa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar Ali Issa na kushoto ni Shaibu Masoud Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Wakulima (AFP).
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakipokea maelezo kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFP)Said Soud katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.
Mhe Said Soud Said akiwahi mkutano wake na Waandishi wa Habari wa Vyombo mbalimbali vya Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa Habari Maelezo Rahaleo.

No comments: