Wasanii wa Kundi la Mjomba Band, wakiigiza kwa kufukuzwa kwa mwanamke aliyekuwa na maradhi ya Fistula, na mumewe ikiwa ni ishara ya kunyanyapaliwa kwa wenye maradhi hayo katika jamii. Onyesho hilo lilifanyika mjini Dodoma jana wakati wa hitimisho ya kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula iliyofanyika katika mikoa mitatu Nchini na kumalizikia katika mikoa ya kanda ya kati mjini Dodoma. Kampeni hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ilikuwa na lengo la kutoa elimu kwa Umma na kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya kati, Mruta Hamisi (aliyesimama kulia) akizungumza wakati wa kuhitimisha kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula iliyofanyika katika mikoa mitatu Nchini na kumalizikia katika mikoa ya kanda ya kati, mjini Dodoma jana.Waliokaa ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii, Dk Stephen Kebwe (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans.Kampeni hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa Umma na kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe (aliyesimama) akizunguza wakati wa kuhitimisha kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula katika mikoa ya kanda ya kati, mjini Dodoma jana. Waliokaa kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Erwin Telemans, Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya kati, Mruta Hamisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UNFPA, Rutasha Dadi. Kampeni hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ilifanyika katika mikoa mitatu ikiwa na dhumuni la kutoa elimu kwa Umma na kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
Wakazi wa manispaa ya Dodoma wakihudhuria kwa wingi kwenye hitimisho la kampeni dhidi ya maradhi ya Fistula. Ambapo Naibu Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe alihitimisha kampeni hizo katika viwanja vya Mashujaa mjini Dodoma jana. Kampeni hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ilifanyika katika mikoa mitatu ikiwa na lengo la kutoa elimu kwa Umma na kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
Wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Stephen Kebwe wakati kuhitimisha kampeni ya maradhi ya Fistula iliyofanyika kwa kuzunguka katika mikoa mitatu nchini na kuhitimishwa katika mikoa ya kanda ya kati, mjini Dodoma jana. Kampeni hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na Hospitali ya CCBRT na Vodacom Foundation ilikuwa na lengo la kutoa elimu kwa Umma na kuwasisitiza wanaume kuwaruhusu wakinamama kujitokeza ili wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Inakadiriwa ni wastani ya wanawake 3,000 kwa mwaka hupatwa na maradhi hayo wanapojifungua.
No comments:
Post a Comment