Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Dkt. Kevin Lothal Mandopi akielezea namna ya tume hiyo ilivyo mstari wa mbele kuelimisha Umma dhidi ya vitendo na ukatili kwa watu wenye Ualbinism nchini kwa wadau na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam mapema leo Juni 13.2015.
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza kwa msisitizo juu ya jamii ya watanzania kuchukua hatua ya kuwalinda watu wenye Ualbinism nchini wakati wa tukio maalum la maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma kuhusu Ualbino, iliyoandaliwa na tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini. kushoto kwake ni Wakili wa Serikali na Mratibu wa masuala ya Albinism nchini, Bi Beatrice Mpangala.
Mkuu wa ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, Bi. Zulmira Rodrigues akizungumza kwa msisitizo juu ya jamii ya watanzania kuchukua hatua ya kuwalinda watu wenye Ualbinism nchini wakati wa tukio maalum la maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Uelimishaji Umma kuhusu Ualbino. kulia ni maafis wa taasisi hiyo ya UNESCO na kushoto kwake ni Wakili wa Serikali na Mratibu wa masuala ya Albinism nchini, Bi Beatrice Mpangala.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi Marry Massay akisisitiza umma kuchukua hatua dhidi ya mapambano kwa watu wenye Ualbinism kwa kuwalinda pamoja na kutoa elimu sahihi ya mapambano ikiwemo kuachana na imani potofu dhidi ya jamii hiyo.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Bi. Neema Ringo,akitoa wito kwa wadau mbalimbali (Hawapo pichani) Kujitokeza katika kesi kutoa ushahidi hasa wakati wa kesi dhidi ya vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watu wenye Albino nchini.ambapo alieleza kuwa wamekuwa na changamoto dhidi ya mashahidi hivyo ni wakati sasa wa wananchi kujitokeza kufuatilia kesi hizo ikiwemo mashahidi kujitokeza.
Mmoja wa wadau waliojitokeza kwenye maadhimisho yaliyoandaliwa na tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini, akichangia maoni yake dhidi ya hatua za kufanyika ili elimu ifike kwa jamii ikiwemo kuwatumia watu mbalimbali hasa ngazi za chini wakiwemo Wenyeviti, madiwani na wakuu wa Wilaya na Mikoa.
Mmoja wa mdau wa masuala ya haki za binadamu, ambaye ni mlemavu, akichangia mada kwenye kwenye maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Taswira katika mkutano huo wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora ukiendelea ukumbini hapo...!
Na Andrew Chale, modewjiblog
Tume ya Haki za binadamu na Utawala bora nchini, leo Juni 13,2015, imeungana na watanzania wote kuadhimisha siku ya Kimataifa ya uelimishaji umma kuhusu Ualbino na haki za watu wenye Ualbino ambapo imeitaka jamii kutambua haki na wajibu wa kuwalinda na kuwathamini.
Akisoma taarifa maalum kwa wadau mblimbali na waandishi wa habari waliojitokeza jijini Dar Es Salaam, Kamishna wa tume hiyo, Dkt. Kevin Lothal Mandopi alieleza kuwa jamii inayo wajibu wa kuwathamini watu hao wenye albinism kwani nao ni kama binadamu wengine na wana haki sawa.
Kamishna Mandopi katika taarifa hiyo alibainisha kuwa, mpango wa elimu kwa umma umelenga kubadilisha fikra, mtazamo na imani potofu juu ya watu wenye ualibinism.
“Ni dhahiri kuwa iwapo jamii itaelewa dhana nzima ya Ualbinism na kubadili fikra na dhana potofu dhidi ya watu hawa, kuna uwezekani mkubwa wa kukomesha kabisa matendo maouvu dhidi ya ndugu zetu wenye Ualbinism” alieleza Kimishna Mandopi.
Kwa upande wake Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Zulmira Rodrigues alisisitiza jamii nchini kuongeza upendo pamoja na kuachana na imani potofu inayosababisha kukithiri kwa vitendo hivyo hapa nchini.
Pia alibainisha kuwa, imefika wakati sasa wa kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ilikutambua wenye Ualbinism ilinao waishi na kupata haki sawa kama binadamu wengine.
“Wajibu wetu ni kuwathamini na kuwalinda watu wenye Ualbinism, tumetembea maeneo mbalimbbali ikiwemo Kanda ya Ziwa katika vituo maalum vya watoto wenye Albinism, Ni wakati wa kuendelea kutoa elimu ili watoto hao watoke huko ili waishi na jamii kama wengine” alisisitiza Bi. Zulmira.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bi Marry Massay alizitaka mamlaka husika ikiwemo za Serikali na watu binafs, vyombo vya habari na jamii kwa pamoja kutoa elimu ya uelimishaji umma kuhusiana Ualbinism ilikuendelea kuwa Tanzania yenye amani na upendo kama ilivyojizolea sifa ndani na nje ya mipaka yake.
Naye Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) Bi. Neema Ringo, alibainisha kuwa, ofisi yake imekuwa mstari wa mbele kufuatilia kesi mbalimbali ikiwemo dhidi ya jamii ya wenye Albinism huku akiwataka wananchi kujitokeza kutoa ushahidi pamoja na kufuatilia kesi hizo mara kwa mara.
Kwa upande wa wadau wengine walitaka Serikali kuwa mstari wa mbele kushikamana na jamii hiyo yenye ualbinism ilikutokomeza kabisa imani potofu iliyojijengeka kwa watu ikiwemo kutoa elimu kwa ngazi zote mara kwa mara.
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ndiye mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya kimataifa ya kuongeza ufahamu juu ya Ualbino ambayo yameandaliwa na Chama Cha Albino Tanzania, jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment