Mtaalam wa Kujitolea
kutoka nchini Japani Bw.Koji Ueda akielezea namna alivyofanya kazi katika shule
ya Sekondari Sogesca iliyoko mkoani Mwanza,katika hafla fupi ya kuwaaga
wataalam wa kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika
ukumbi wa Utumishi leo.
Mtaalam wa Kujitolea
kutoka nchini Japani Bi. Haruka Ota akielezea namna alivyofanya kazi katika
Maktaba Kuu ya Taifa,wakati wa hafla fupi ya kuwaaga wataalam wa kujitolea
kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo.
Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japani waliomaliza muda wao wa kutoa huduma nchini wakimsikiliza
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Utumishi Bw.HAB Mkwizu katika hafla fupi ya
kuwaaga iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais-Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kushoto) akikabidhi zawadi kwa Mtaalam wa
Kujitolea kutoka nchini Japani Bi.Sekiko
Masui aliyemaliza muda wake wa kutoa huduma nchini
katika hafla ya kuwaaga wataalam hao iliyofanyika ukumbi wa Utumishi leo
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya
Rais- Utumishi Bw.HAB Mkwizu ( wa tatu kutoka kulia) akiwa katika picha ya
pamoja na Wataalam wa Kujitolea kutoka nchini Japan waliomaliza muda wao wa
kutoa huduma nchini baada ya hafla ya kuwaaga iliyofanyika ofisini kwake leo. Wengine
ni watumishi wa Ofisi ya Rais-Utumishi na Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
No comments:
Post a Comment