Mh. Samia Suluhu Hassan
Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Mh John Pombe Magufuli amemtangaza mgombea mwenza wake kuwa ni Mh. Samia Suluhu Hassan.
Mh Magufuli amemtangaza Mh Samia wakati alipokuwa akikishukuru chama chake kwa kumteua kuipeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao baadaye mwaka huu.
Baada ya kumtangaza Mh Samia kuwa mgombea mwenza wake, ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe na vigelele.
Hii ni mara ya kwanza tangu uhuru kwa Tanzania kuwa mgombea mwenza mwanamke.
No comments:
Post a Comment