ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 4, 2015

Hongera Sana Dr. Slaa


Katika kila mwanadamu anayejitambua lazima atakuwa na kitu kinaitwa “core principles.” Yani hizi ni kanuni kuu za msingi wa maisha yako ambazo zinakupa ‘identity’ ya wewe ni nani au mtu wa namna gani! Hizi si misingi au miiko uliyo jiwekea tuu kwasababu ya kujifurahisha, hapana! Ni misingi na miiko unayoiyamini na hukotayari kuisimamia bila kutetereka kwa gharama yoyote ile. Haijalishi hata kama watu wote watakuona wewe ni mtu wa ajabu, lakini kwako itakuwa salama rohoni mwako kwasababu hizo ni principle zako za maisha umejiwekea, unaiyamini, na hupo teyari kuitetea mpaka kufa! “A man who stands for nothing will fall for anything”-Malcolm X. Mtu ambaye hana msingi au miiko katika maisha yake ni mtu ambaye hajitambu na wala hajui dhamani yake! Nandiyo maana watu kama hawa wanaweza leo wakasimama na kutowa kauli kali kwenye kadamunasi kama “over my dead body” lakini kesho bila aibu wala soni usoni akafanya kile kile ambacho alikanusha kuwa hawezi kufanya unless it’s over his / her dead body! SMH!

Misingi na miiko mbayo mtu anajiwekea ndizo zimefanya baadhi ya watu wameitwa “Pioneers” wa kitu fulani. Iwe kwenye siasa, imani za kidini, au mambo ya kijamii kuna pioneers wa aina mbali mbali na watu tunawangalia kama kioo au role-model! Watu wanao jitambua pamoja na pioneers watakwambia kunavitu ambavyo siwezi ku-compromise hata kidogo, kwa mfano wapo wengi atakwambia mie hata sikumoja siwezi ku-compromise my core-principles; na moja ya misingi yao nikujali sana UTU NA HESHIMA yao! Sikuzote utu na heshima yao vitakuja kwanza kabla ya kitu kingine chochote kile (his / her dignity and respect will always comes first no matter what!). Mtu anaweza kuwa yupo teyari kuacha kila kitu kipotee hata kama anaonewa ili kulinda utu na heshima yake. Inaweza ika-sound crazy to other people lakini hii ndiyo miiko au misingi yake aliyojiwekea na yupoteyari kuisimaimia kwa gharama yoyote ile. Soma Zaidi

10 comments:

Anonymous said...

Ebu tupishi sisi. Hizo princciple hazina kichwa wala miguu. Ebu tuanza na hizo core value. Waribo yupo fungu gani? CCM wamechanachana maoni ya wananchi.Mbona yupo huko huko CCM?

Anonymous said...

Afadhali kuna mtu anaesimamia maadili kwa heshima ya wanyonge wasiokuwa na wakuwasemea,inapofika wakati kiongozi mwenzio hajali msimamo wako na anaropoka kuwa liwalo na liwe au apumzike atatukuta mbele ya safari inaonyesha kuna watu wana walakini katika utu na hawachagui cha kuongea.Slaa apewe heshima yake hata kama anamapungufu yake

Anonymous said...

Mpendwa, sijui nikupishe uwende wapi maana mie nipo kwangu! Na upo na nani katika hiyo safari yako?

Sijaelewa point yako, labda ufafanue....

Mie sijaongea chama nimeongelea mtu.....na hata kama ni Judge Warioba pamoja na vurugu na mizengwe aliyo fanyiwa umeona amebadili msimamo wake kuhusu Katiba?? Na hicho ndicho ninacho kiongelea! Kuwa na msimamo kwa kile unacho kiamini kuwa ni sahihi!

Natumia utakuwa umenielewa!

Anonymous said...

Brave man and smart.

Anonymous said...

twende mbele na kurudi nyuma na kusema ukweli huyu Dr. Slaa angesimamishwa CCM wangechukua nchi kilaini sana. hivyo hata yeye anajijua hawezi kuindoa ccm madarakani angeweza kuwa hata PM hivyo inabidi kuacha kumsikiliza mkewe kwa kiasi hiki.

Anonymous said...

Dr. Slaa hesabu yake ilikuwa ni kuwapa masharti viongozi wengine kwamba yeye akigombea na akashindwa, wamlipe kila mwezi. Tena analipwa kiwango kikubwa sana. Alifanya hivyo uchaguzi uliopita. Anajua vizuri hawezi kushinda maana alisimamishwa na Kikwete, akapoteza. Sasa Magufuli yupo better. Ni sawasawa na kufungwa na timu ya polisi mabao 5-0 ukatarajia kuifunga Arsenal.
Kina Mbowe walishajua janja yake. Yaani ni kukielemea chama bila aibu. Hivyo wakampumzisha. Mchaga huyo!

Anonymous said...

"After leaving the Nation of Islam in March 1964, he made Hajj, which helped change his perspective on whites and racism completely."

NIMEAMUA KUWEKA HIYO QUOTE HAPO JUU KUMUONYESHA MWANDISHI KWAMBA THERE WERE TWO MALCOLM X AND HIM BEING A CHANGED MAN AFTER HIJJA DID NOT TARNISH HIS REPUTATION THE WAY POOR MINDED PEOPLE ARE TRYING TO DO WITH LOWASSA. POLITICS IS THE GAME OF THE MOMENT AND TIMING IS THE KEY. IF YOU MISS YOUR MOMENT THAT'S IT. LET'S ALL AGREE FOR A SECOND THAT "FORGET ABOUT MBOWE, LIPUMBA, SLAA or MAALIM" LOWASSA IS THE TALK OF THE TOWN AND WHOEVER TOOK THEIR CHANCES OF HAVING HIM ON THEIR PARTY "FOR THIS CASE CHADEMA" WILL DEFINETELY BENEFIT BIG TIME. THE ONLY QUESTION WE NEED TO ASK OURSELVES IS, HOW LONG WILL HE LAST? NOBODY KNOWS... AND THAT'S WHY IS CALLED TAKING CHANCES.

Anonymous said...

There is a lot of Cowards people on CCM

Anonymous said...

Dr Slaa ana maadili na core principles Mwenyekiti wake hana na ni fisadi ndani ya chama

Anonymous said...

Huyu bwana si mtu wa principles: Kaacha upadri ili aoe; kaachika ili aoe eti mwanamke mwenye hadhi ya juu kuingia naye Ikulu (kulingana na maneno yake mwenyewe)! Huyu ni mtafuta makuuu, tu!