Tuesday, August 18, 2015

MASANJA MKANDAMIZAJI ATEMBELEA SamSPRO Studio WASHINGTON, DC

Mhubiri wa kimataifa na mchekeshaji maarufu Emmanuel Mgaya au jina maarufu Masanja Mkandamizaji juzi alitembelea studio za kuzalisha muziki na video za SamSPRO Studios zilizoko Washington, DC. Masanja kama anavyoonekana kwenye picha aliambatana na waimbaji wa nyimbo za injili Milca Kakete kutoka Canada na Milca Thomas kutoka North Carolina, pamoja na baadhi ya waimbaji wa kundi la The Sound of Glory kutoka kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries lililoko Washington DC ambako mwigizaji huyo maarufu alikuwepo kama mhubiri mkuu wa mkutano uliokuwa ukiendelea kwa siku tatu mfululizo. Akijibu swali alipoulizwa juu ya ugeni huo studioni hapo producer na mmiliki wa studio hiyo ndugu Samuel Malonja alisema kuwa Masanja aliamua kutafuta studio ambayo anaweza kuitumia kurekodi wimbo wake, hilo ndio lilikuwa lengo la ugeni huo. Masanja amerekodi wimbo mmoja katika studio hiyo akiwashirikisha waimbaji wengine wa injili akiwemo Milca Kakete kutoka Canada, Milca Thomas kutoka North Carolina na waimbaji wa kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries la mjini Washington DC. Picha hapo chini zinaonyesha kazi ya kurekodi wimbo huo chini ya producer Sam ikiendelea huku Masanja akionekana kusimamia zoezi hilo kwa umakini kabisa.

4 comments:

Anonymous said...

Hajafikia kuitwa wa kimataifa

Anonymous said...

Kweli mablogers mna makuzinya mambo! Ni kigezo gani kimefanya aitwe wa kimataifa. Wakati wale waimbajinwake tunawajua kwa maadili.mabovu hapa si DC, Ohio, Florida, California na NewYork. Ni vyema mkaandika kwa kiasi lakini.mkizidi inabidi tuseme yanayoonekana.!!

Anonymous said...

Aisee mangi mbona unawivu usio na maana hata akiitwa wa ulimwengu wewe unapoteza nini acha kuwa na wivu nanii ukitaka na wewe siuanze kituchapa injili arawa

Anonymous said...

One of my favorite studios