ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 4, 2015

Msanii maarufu wa Bongo movie, Irene Uwoya ameshinda kura za maoni Ubunge Viti Maalum(vijana)Tabora, kwa tiketi ya CCM


Msanii maarufu wa Bongo movie, Irene Uwoya ameshinda kura za maoni Ubunge Viti Maalum(vijana)Tabora, kwa tiketi ya CCM

-Amepata kura 38 huku mpinzani wake akipata kura 34
Tarime Mjini na Tarime Vijijini zoezi la kupiga kura limeahirishwa
Kumetokea vurugu kwenye mchakato wa kura za maoni CCM hapa Tarime, kwani zimekutwa karatasi za kupigia kura zaidi ya 25000 zikiwa zimeshatikiwa majina ya wagombea wawili MH GAUDENSIA KABAKA (TARIME MJINI) na NYAMBARI NYANGW'INE (TARIME VIJIJINI).
Kutokana na kadhia hiyo uchaguzi usogezwa mbele hadi kesho, wanachama wamehoji uhalali wa hizo makaratasi zilipotunzwa na kuleta vurugu japo hakuna majeruhi yaliyotokea miongoni mwa wanachana (wajumbe).
Mytake: CCM HAMFUNDISHIKI WALA KUJIFUNZA


CHANZO: MIMI MWENYEWE

By lengume
Mtu mmoja amekamatwa akiwa ktk harakati za kuingiza kura zilizotikiwa tayari kwenye box la Kura.


Katika kata hii ya Kaloleni wagombea wenye upinzani mkubwa ni Tojo na Seif Simba.


Kura zilizokamatwa zilitikiwa jina la Seif Simba.


Baada ya vurugu kutokea mjumbe wa halmashauri kuu Ndugu Godfrey Mwalusambo aliweza kumuokoa Mtu huyo na kumpeleka Polisi.

MORE UPDATES:

Kigamboni Ndugulile kashinda kwa 80%


Nape kashinda kwa kishindo


SEGEREA
Mbunge:BONA KALOA 
Diwani: SOUD MOHAMED SOUD
(Mbunge ni mwanamke)


Ulanga Mashariki, Mbunge Celina kombani


Ilala ameshinda Zungu


Ukonga mshindi ni Ramesh Patel


Bumbuli
1.January - 13,366~87%


Nzenga Mjini Bashe kashinda kwa asilimia 99%...


Sengerema: William Ngeleja 


Nyamagana: Mabula 


Butiama: Mkono


Morogoro mjini: Abood

By Meek Mill
KURA ZA MAONI CCM
1. Mwigulu - Iramba


2. Nape - Mtama


3. Mwakasaka - Tabora Mjini


4. Mama Sitta - Urambo


5. Kadutu - Ulyankulu


6. Bashe - Nzega


7. Ngeleja - Sengerema


8. Seif - Igunga ktk jimbo jipya.


9. Masaburi - Ubungo


10. Patel - Ukonga


11. Prof Kamala - Nkenge, Misenyi


12. Kagasheki - Bukoba mjini


13. Lukuvi - Isimani


14. January - Bumbuli


15. Muhongo - Musoma vijijini


16. Ndugai - Kongwa


17. Chumi - Mafinga


18. Kigola - Mufindi kusini


19. Mgimwa - Mufindi kaskazini


20. Filikunjombe - Ludewa


21. Mgimwa - Kalenga...


22. Lusinde - Mtera


23. Imani Moshi - Kaliua


24.Mwakasaka -Tabora mjini


25.Fenala Mkangara -Kibamba


26.Mapunda-Mbinga mjini


27.Masele -Kahama


28.Antony Mavunde-Dodoma 


30. Mosha Davis Elisa-Moshi Mjini




By Magazetini
Bunda:Stephen Wassira atangazwa mshindi chini ya ulinzi Mkali wa Polisi


Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Bunda, Stephen Wasira ametangazwa kushinda kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya ulinzi mkali polisi.


Matokeo hayo ambayo yametangazwa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe na msimamizi wa uchaguzi wa CCM, Margret Mtatiro alisema Wasira ameshinda kwa zaidi ya kura 223 baada ya kupata jumla ya kura 6,429 akifuatiwa na Robert Maboto (6206), Christopher Sanya (1140), Exavari Lugina (846), Simon Odunga (547), Magesa Mugeta (446), Peres Magiri (385) na Brian Bita (263).


Matokeo hayo yalitangazwa jana majira ya saa 4 alasiri baada ya mvutano mkali tangu juzi usiku, ambapo ilidaiwa kuwa baada ya kujumlisha kura zote mpinzani wake Robert Maboto alionekana kumzidi Wasira kwa kura 67.


Hata hivyo kutokana na Wasira kutoridhika, uhakiki ulirudiwa tena ambapo majira ya saa 4 asbuhi jana Jeshi la polisi lilifika katika ofisi za CCM na kuweka ulinzi dhidi ya wapambe wa Maboto ambao walionesha wasiwasi wa Maboto kuporwa kura zake.


Kabla ya Polisi kufika katika eneo hilo, mkuu wa wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe alionekana katika ofisi hizo akifanyakazi kubwa ya kutuliza wafuasi wa Maboto ambao walikuwa wakiimba, ‘Maboto ni mbunge’, Maboto ni Mbunge”.


Hadi Matokeo yanatangazwa Mkuu huyo wa Wilaya alionekana akiingia na kutoka mara kwa mara ndani ya ofisi hizo ambazo shughuli za uhesabuji kura zilikuwa zikifanyika jambo ambalo halikuwaridhisha wapenzi wa wagombea wengine.


Pamoja na hayo Wakala wa Maboto aliyejitambulisha kwa jina moja la Chang’ang’a alikiri kuwepo mizengwe katika kurudia mahesabu ya kura hivyo yeye na Maboto wamesaini kutoridhwa na matokeo hayo.


Akizungumza baada ya kutangazwa mshindi huku wanachama wengine wakipiga kelele kwa kutoridhishwa na matokeo hayo , Wasira alisema bado jimbo la Bunda mjini halijapata mgombea mpaka majina matatu ya washindi yatakapojadilliwa na halmashauri kuu ya CCM taifa(NEC).


“Sasa CCM ni mamoja, hapa sasa hakuna kikundi cha Wasira wala Maboto, tumepata mgombea mmoja atakayepambana na UKAWA, lakini mpaka majina yote yakajadiliwe katika halmashauri kuu ya CCM,” alisema Wasira.


Baada ya matokeo hayo mamia ya wanachama ambao hawakuonesha kuridhwa na mchakato wa utangazwaji wa matokeo hayo walichana kadi za CCM na kuimba Ukawa huku wakidai CCM imekuwa ikiwaletea wananchi wagombea wasiowakubali hivyo watajiunga na UKAWA.


1. Kilimanjaro


Jimbo la Moshi Mjini
Davis Mosha kura 5,271 sawa na asilimia 75, Patrick Boisafi 767, Buni Ramole 439, Halifa Kiwango 122, Michael Mwita 118, Priscus Tarimo kura 94, Daudi Mrindoko kura 65, Amani Ngowi kura 47, Omary Mwariko kura 27, Shanel Ngunda kura 20, Edmund Rutaraka kura 14 na Innocent Siriwa kura 13.


Jimbo la Moshi Vijijini
Cyiril Chami ametetea kiti chake kwa kupata kura 5,610 sawa na asilimia 53.84, akifuatiwa na Ansi Mmas 3,181 sawa na asilimia 30.53, Victor Tesha 834 sawa na asilimia 8.00, Emmy Chiduo 421 sawa na asilimia 4.04 na Thomas Ngawaiya 373 sawa na asilimia 3.58.


Jimbo la Vunjo
Innocent Shirima ameongoza kwa kupata kura 4,541,akifuatiwa na Dk. Msafiri Mbaga 1,457, Veronica Shao 1,178, Eveline Msangi 831, Peter Msack 632, Masiga Amos 460, Mchungaji Alphonce Temba 416 na Joachim Kessy 147.


Jimbo la Hai
Dastan Malya ameongoza kwa kupata kura 8,250, akifuatiwa na Maynard Swai kura 2,512, Fuya Kimbita 2,275, Gasper Ngido 809 na Judicate Lyatuu 212


Jimbo la Siha
Aggrey Mwanry ametetea kiti chake kwa kupata kura 12, 893 na Anael Nanyaro kura 1,875.


Jimbo la Rombo
Colman Samora kura 4,481, Evod Mmanda kura 1,906, Notiburga Maskini kura 1,567, Calist Silayo 694, Emmanuel Kavishe kura 650, Boniphace Kavishe, kura 515, Paul Massawe kura 96, na Gabriel Meela kura 95.


2. Morogoro


Morogoro Mjini
Aziz Abood kura 20,094, GSimon Berege kura 429.


Mlimba
Godwin Kunambi kura 6233, Dk. Frederick Sagamiko kura 2203 na Jane Mihanji kura 2073.


Ulanga
Celina Kombani kura 12,036, Augustino Matefu kura 2,736 na Kitolero Daud kura 194


Gairo
Ahmad Shabiby alipata kura 15,920, Omary Bawazir alipata kura 886 katika kata 16 kati ya 18.


3. Pwani


Kibaha
Humoud Jumaa ameshinda kwenye kura za 6,941, Hussein Chuma kura 1,161, Alen Bureta kura 894, Janeth Munguatosha 126 na Shomary Sangali kura 99.
Katika kinyang’anyiro hicho kilishirikisha wanachama 10,387, ikiwa na wagombea sita, waliojiandikisha ni 16,636, huku waliopiga kura ni 10,387.


Chalinze
Ridhiwani Kikwete ameshinda kwa asilimia 89, 


Bagamoyo
Dk. Shukuru Kawambwa akishinda kwa asilimia 36.


4. Tabora


Tabora Mjini
Wabunge wakongwe, Ismail Rage wa Jimbo la Tabora Mjini, Mhandisi Athuman Mfutakamba wa Jimbo la Igalula na Shafir Sumar wa Jimbo la Tabora Kaskazini, wametupwa nje ya kinyang’anyiro hicho.Mgombea Emmanuel Mwakasaka alipata kura 11,280, Rage kura kura 3,380.


Igalula
Musa Ntimizi anaongoza kwa kura 7,200, Athuman Mfutakamba alipata kura 3,500 na Hanifa Kondo alijipatia kura 3,200.


Tabora Kaskazini
Almas Maige anaongoza, Shafin Mamlo Sumar alipata kura 6,394 na Joseph Kidaha kura 5,694.


Ulyankulu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, John Kadutu, anaongoza kwa kura 13,600, Dk. Msonde Sydney kura 1,167.


Urambo Mashariki
Mke wa Spika wa zamani, Samuel Sitta, Magreth Sitta anaongoza kwa kujinyakulia kura 12,392 na Ali Maswanya kura 4,175.


Bukene
Suleiman Zedi alipata kura 12,894, Deo Kahumbi kura 2,728, na Tedy Kaselabantu alipata kura 1,441.


Sikonge
Mbunge wa zamani, Said Nkumba, anaongoza dhidi ya mpinzani wake.


5. Manyara


Kiteto
Mjumbe wa Halmshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Emmanuel Papian, anaongoza kata 20 kati ya 23 zilizopo wilayani humo, alipata kura 37,636, Benedict ole
Nangoro, mbunge anayemaliza muda wake alipata kura 21,471.Hajjat Amina Mrisho kura 2,133, Ally Lugendo kura 288 na Joseph Mwaleba alipata kura 261 Kata ambazo matokeo yake hayajawasilishwa ni Namelock, Makame na Ndirigish.


Hanang
Dk.Mary Nagu aliibuka mshindi kwa kupata kura 21,837, Peter Nyalandu 5,558, Dancun Mayomba kura 4753.


Babati Mjini
Kisieri Chambili alipata kura 3,722, Ali Msuya kura 1,758, James Darabe kura 904.


6. Arusha


Arusha Mjini
Mfanyabiashara maarufu Philemon Mollel aliibuka mshindi, lakini matokeo hayo yalipingwa na mfanyabiashara Justine Nyari, aliyedai kuwa alitumia rushwa, hila na ukabila.


Katika uchaguzi huo, wanachama 12 waliojitokeza kuwania nafasi hiyo, matokeo yanaonesha Mollel aliibuka kidedea kwa kupata kura 5,320, akifuatiwa na Justine Nyari aliyepata kura 1,894, Mosses Mwizarubi kura 1,105, Thomas Munisi kura 832 na Victor Njau 752.Wengine ni Walehe Kiluvia kura (446), Hamisi Migire kura (305), Edmund Ngemera (198), Ruben Mwateni kura(171), Emmanuel ole Njoro (90) na Mahmudu Omari (90).Nyari alisema katika Kata ya Elerai wapiga kura walikuwa 250, lakini waliopiga kura juzi katika kituo walikuwa 733 na kumpa Monaban kura 467, kitu ambacho alidai ni udanganyifu.Alisema ana ushahidi wa kata nyingi zilizofanywa hivyo na kwamba, atawasilisha malalamiko yake kwa viongozi wa juu wa chama ili kuangalia namna gani hatua za kinidhamu zitaweza kuchukuliwa dhidi ya kada huyo aliyedai kukipaka matope chama.


“Ametengeneza fulana zilizokuwa zimeandikwa ‘mtashinda lakini hamtashinda nyingine, kamanda wetu ndiyo kiongozi wetu, na nyingine zilisema chagua Lowassa, chagua Monaban”….Nimemwandikia barua Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na kumweleza kila kitu kilichokuwa kikiendelea, kabla ya kampeni na ndani ya kampeni, nasubiri majibu na nina imani na chama kuwa, watayafanyia kazi malalamiko hayo,”alidai.


Nyari alisema mbali ya hilo, pia alitumia ukabila katika kata za Terat, Muriet, Olmot, Olasiti, Moivaro, Moshono na Osunyai kwa kuwaapiza kula nyama ya ng’ombe wapiga kura wa CCM. Hatua hiyo wapiga kura hao waliogopa kuwapa kura makada wengine hatua ambayo ni mbaya ndani ya chama.


Monduli
Mtoto wa Marehemu Sokoine, Namelock Sokoine ameshinda kwa kura 29,582 akifuatiwa na Loota Sanare aliyepata kura 8860, Lorinyu Nkosi kura 235, Mbayani Tayani kura 226, Amani Torongei kura 107 na Sakaya Kabuti aliyepata kura 159.


Arumeru Mashariki
Kamanda wa vijana wilaya hiyo, Danielson Pallangyo ‘Jdee’ alipata ushindi wa kura 11,342, Siyoi Sumari kura 3,491, Willium Sarakikya aliibuka na kura 3,159, Dk. Daniel Pallangyo aliyepata kura 1,646, Elirehema Kaaya kura 818 na Angel Pallangyo kura 321 na Mhoho Jackson akipata kura 178.


Karatu
Dk.Wilbard Lori aliibuka kidedea kwa kupata kura 17,711, Rajabu Malewa, aliyepata kura 911 na nafasi ya tatu kuchukuliwa na John Dodo aliyepata kura 745 na Josha Mbwambo kura 67.


7. Mwanza
Mchuano wa kuomba ridhaa ya kupendekezwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwania ubunge mikoa ya Kanda ya Ziwa, unaonesha baadhi ya mawaziri wa Serikali, wakipenya katika kura za maoni, huku wengine wakongwe wakibwagwa.


Waliopeta ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk. Charles Tizeba na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Lakini, hali ilikuwa mbaya kwa Lawrance Masha waliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alitupwa nje katika Jimbo la Sengerema, ambapo Ngeleja aliibuka anaongoza.


Misungwi
Charles Kitwanga ameibuka mshindi kwa kupata kura 26,171, Jacob Shibiliti alipata kura 7, 009, Shomari Emmanuel kura 1,840, Dk Makene Madoshi kura 1,339 na Cleophas aliyepata kura 1051.


Buchosa
Dk.Tizeba alikuwa akiongoza kwa kupata zaidi ya kura asilimia 65 dhidi ya mpinzani wake, Eston Kasika.


Kwimba
Mafuriko ya Shanif Mansoor yamewazoa na kuwatosa wagombea wenzake akiwemo, Bujiku Sakila, Naibu Waziri wa Elimu wa zamani na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, ambaye alipata kura 1,594, sawa na asilimia 1.95.Mansoor alipata kura 13,099, Robert Gwanchele aliambulia kura 1,182.


Sumve
Richard Ndassa ameendelea kumtambia Gabriel Mchele, baada ya kumbwaga kwa kura 11,883. Mchele ambaye awamu iliyopita alishindwa na Ndasa, kura zake zimepungua na kuishia 6,427.


Nyamagana
Stanslaus Mabula aliyekuwa Meya wa jiji hilo na Diwani wa Kata ya Mkolani, amewabwaga vibaya wagombea wenzake, akiwemo Raphael Shilatu na Joseph Kahungwa waliopata kura kidogo.Mbali na vituo viwili vya Mkuyuni kuahirisha kupiga kura juzi, hadi tukienda mitamboni vilikuwa vikiendelea kupiga kura, Mabula amevuna kura 8,738 na kutuma salamu za kumg’oa Wenje, akifuatiwa na Kahungwa aliyepata kura 3,074.Shilatu alipata kura 922 na Robert Masunya aliyepata kura 944.


Ilemela
Mkuu wa wilaya ya Iringa Vijijini, Angelina Mabula, ameongoza jimbo hilo kwa kura 6,324, Barnabas Mathayo kura 3,562, John Buyamba kura 1,167, Stephen Magoiga alipata kura 1,064, na mtangazaji wa ITV, Godwin Gondwe akishika nafasi ya tano kwa kupata kura 827.


Ukerewe
Christopher Nyandiga ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, aliongoza kwa asilimia nyingi.


8.Geita


Chato
Dk. Medard Kalamani amejikatia tiketi ya kumrithi Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ambaye anapeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya urais.
Dk. Kalamani alipata kura 12,892 kati nya kura halali 23,892, Deusdedith Katwale kura 3,251, Saimon Michael alipata kura 2,150 na Alphonce Chandika kura 1,244.


9. Simiyu
Busega
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Dk. Titus Kamani na Raphael Chegeni waliochuana vikali.Dk. Kamani alipata kura 10,697 Dk. Chegeni kura zaidi ya 9,661, lakini amepinga matokeo hayo.


Magu
Desdery Kiswaga, alikuwa akiongoza kwa kupata asilimia zaidi ya 70 na kuwapiku wapinzani wake, Felician Shejamabu, Mhandisi Leonard Kadashi na Sixbert.


Meatu
Salum Mbuzi anaongoza kwa kura 13, 180, Oscar Maduhu, kura 2,988, Lomano Thomas alipata kura 358 na Donard Ginasa kura 350.


Itilima
Mjumbe wa NEC, Njallu Silanga, alipata kura 44,486, Simon Ngagani kura 2,759 na Danhi Makanga, aliyepata kura 814.


10. Dodoma


Dodoma Mjini
Anthon Mavunde anaongoza kwa kura 8,584 katika kata 23 kati ya 41 za Dodoma Mjini, akifuatiwa na Hidery Gulamali mwenye kura 5,526.
Mbunge anayemaliza muda wake, Dk.David Malole, alishika namba tatu akiwa na kura 2,156, Musa Luhamo kura 2,076, Robert Mtyani kura 2009, Anthon Kanyama kura 1,847, Emmanuel Kamala 1,178, Steven Masangia 929, Mihamed Mgoli 351, Mruke Mruke kura 195.


Chemba
Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia, ameibuka kidedea katika kura za maoni za ubunge CCM jimbo la Chemba mkoani Kondoa.
Matokeo ya awali yanaonesha kuwa, mshindi ni Nkamia, lakini msimamizi alikataa kuwataja wanaofuatia kutokana na kuendelea kukusanya matokeo.


Kongwa
Kwa upande wa Jimbo la Kongwa, Naibu Spika Job Ndugai ameibuka kidedea dhidi ya wapinzania wake licha ya kucheza rafu katika mchakato wa kampeni.
Kwa mujibu wa Augustine Minja, hayo ni matokeo ya awali ambayo yanaonesha Ndugai anaongoza katika jimbo hilo dhidi ya wagombea wenzake wanane.


Kibakwe
Katika jimbo la Kibakwe Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachaweni ameibuka kidedea katika kura za maoni na kuwabwaga wagombea wenzake.
Kwa mujibu wa msimamizi wa uchaguzi, Ndaluone Mbogo, alisema katika kura hizo za maoni kwa matokeo yaliyokusanywa mpaka sasa inaonesha wazi kuwa, Simbachawene ndiye mshindi kwa nafasi ya ubunge.


Mtera
Katibu wa wilaya ya Chamwino Janet Mashele alisema Mbunge anayetete nafasi yake Livingstone Lusinde anaongoza katika jimbo hilo kwa matokeo ya awali.


Mpwapwa
Katika jimbo la Mpwapwa, George Lubeleje ameibuka kidede kwa kumshinda aliyekuwa akitetea jimbo hilo, Gregory Teu.
Lubeleje ambaye aliwahi kuwa mbunge wa jimbo hilo miaka ya nyuma hadi 2010 alipoangushwa na Teu ameikwaa nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitano ya kuwatumikia wananchi wa Mpwapwa.


Bahi
Jimbo la Bahi aliyekuwa akitetea jimbo hilo, Omary Badweli, ameibuka kidedea kwa kuwashinda wapinzani wake.
Kwa upande wake Katibu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Arbert Mgumba alisema mpaka sasa hajapata matokeo kamili kutokana na kuwepo kwa changamoto nyingi za ukusanyaji wa matokeo na jiografia ya wilaya hiyo.


Kondoa vijijini
Kwa upande wa Kondoa Vijijini, Hassan Lubuva, ameibuka
mshindi katika mchakato huo wa kura za maoni.


Kondoa Mjini
Katibu wa wilayani humo, Shekue Pasua alisema matokeo ya awali Mbunge anayetetea nafasi yake Zabein Mhita anaongoza, huku akifuatiwa na mpinzani wake Edwin Sanda.Aidha alisema,matokeo ya vituo vingi katika wilaya hiyo bado hayajafika wilayani kutokana na jiografia ya eneo hilo.


11. Shinyanga


Shinyanga Mjini
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais anayehusika na Muungano, Steven Masele alipata kura 7,900, Dk. Charles Mlingwa kura 669, Erasto Kwilasa kura 232 na Tara Mzeima alipata kura 43.


Msalala
Aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige ameshinda jimboni mwake kwa kura 11, 575, Emmanuel Kipole kura 1197, John Sukiri kura 962, Nicolaus Mabwa kura 668, Maganga Mashalla kura 597, John Rufunga kura 294 na Wankia Walema kura 14.


Kishapu
Suleiman Nchambi aliibuka mshindi wa jimbo hilo.


Solwa
Ahmed Salimu aliibuka kidedea jimboni kwake.


Kahama Mjini
Jumanne Kishimba alitoka kifua mbele jimboni kwa kura 9754, Charles Nkuba (1301), Godwin Kintoki (433), Mareo Bundalla (284), Kambarage Masubo (280), Deogratias Sazia (257), Robert Kapera (135), Gerald Huhende (106), Malele Charles (91), Tange John (78), Deogratius Mpagama (57), Machunde Eliakim (56) na Masanje Andrew (48).


Ushetu
Elias Kuandikwa alishinda jimbo hilo jipya, Charles Shigino, alijitoa na kukimbilia Chadema, baada ya kuona mchakato ndani ya chama hicho kughubikwa na sintotahamu kwa kutuhumiana baadhi yao kutoa rushwa kwa wanachana wa chama hicho.
Elius Kuandikwa (11,550), Isaya Bukakiye (5241) na Elias Mlyasi kura (207).


12. Mara
Bunda
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, ameshinda kwa kupata kura 6,429, Robert Maboto aliyepata kura 6,206.
Christopher Sanya alipata kura 1,140, Exavery Lugina aliyepata kura 846, Simoni Odunga kura 547, Magesa Mugeta alipata kura 446, Peres Magir kura 385 na Burian Bitaa kura 263.


Mwibara
Kangi Lugola ameshinda uchaguzi katika kura za maoni za chama hicho na kumshinda kwa kura nyingi mpinzani wake wa karibu, Charles Kajege, aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo.


Musoma Vijijini
Profesa Sospeter Muhongo amepeta katika kinyang’anyiro hicho.


Butiama
Nimrod Mkono alikuwa anaongoza katika kata 18 za jimboni humo.


Serengeti
Naibu Waziri wa Afya, Kebwe Stephen, amepita bila kupingwa katika jimbo hilo.


13. Kagera


Biharamulo
Oska Mukasa alipata kura 8,564, Zyun Hussein kura 2,192, Anatory Choya kura 1,339, Dk. Magnus Banyikira kura 759, Paul Kamhandakura 379, Agricola Magoho kura 339.


Bukoba Mjini
Khamis Kagasheki kura 6,971, Anatory Amani alipata kura 944, George Rubaiyuka kura 113, Josephat Kaijage kura 71, Mujuni Kataraiya alipata kura 53, Philbert Katabazi kura 34, Christine Rwezaula alipata kura 29 na Herieth Projestus aliyembulia kura 19.


Ngara
Alex Gashaza aliongoza kwa kupata kura 10,814, Issa Samma kura 7,166), Hellena Ghozi kura 5474, Dk.Philimon Sengati kura 4,393, Gerad Muhile kura 1,866, Cyprian Muheranyi alipata kura 927, Ladslaus Bambaza kura 636, Wilbard Ntamahungiro alipata kura 390 na Joackim Nchunda alipata kura 357.


Muleba Kusini
Profesa Anna Tibaijuka aliibuka kidedea kwa kura 1,7429, Muhaji Basheko kura 3,349, Bravius Kahyoza kura 2,489, Dk. Adam Nyaruhuma (alipata kura 1,445, Mnawaru Amoud kura 1,382, Steven Tumaini kura 531, Mhandisi Buruan Rutabanzibwa alipata kura 481, Eric Raulian kura 171 na Gidion Mandes kura 160.
Muleba Kaskazini Charles Mwijage kura 20,706 na Ambrose Nshallah kura 3,573.


Nkenge
Dk. Diodorus Kamala kura 8,229, Florent Kyombo alipata kura 5,609, Asumpta Mshama kura 5,273, Julius Rugemalira kura 5,198, Dk. Joackim Kamazima alipata kura 2093 na Dk. William Nyagawa.


Karagwe
Innoncet Bashungwa aliibuka mshindi kwa kupata kura 19,990, Audax Rukonge kura 2,209, Alfred Rujwauka aliibuka na kura 1,522, Amon Chakushemale kura 1,072, Dagobat Tigalyoma kura 792 na Kamhangile Mjungu alipata kurta 508.


Majimbo ya Kyerwa na Bukoba Vijijini matokeo yake hayakutangazwa, lakini Bukoba Vijijini ziliibuka vurugu, hivyo watapiga kura leo.


14. Mbeya


Mbozi, 
Naibu Waziri wa Kilimo na Ushirika, Godfrey Zambi ameibuka kidedea kwa kutetea nafasi yake baada ya kupata kura 11,286, George Mwanisongole aliyepata kura 4,558, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima alipata kura 2,956.


Vwawa
Japheti Hasunga alipata kura 10, 902, Mchungaji Tito Nduka kura 3,911, huku watatu akiwa ni Dismas Haonga aliyepata kura 2,205.


Kyela
Dk. Mwakyembe aliibuka mshindi kwa kupata kura 15,516, George Mwakalinga kura 4,905 na Gabriel Kipija kura 2,301.


Rungwe
Richard Kasesela alipata kura 8,596, Amon Sauli kura 8,562, Akim Mwambene aliyeambulia kura 2,569.


Mbeya Mjini
Sambwee Shitambala kura 4,633, Amani Kajuna kura 4,409


Ileje
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, alifanikiwa kumwangusha Aliko Kibona, Wilman Ndile, Mercilin Ndimbwa, Liaison Mkondya na Godfrey Msongwe.


15. Lindi
Mtama
Nape Nnauye ameshinda kwa kupata kura 16,105, Suleiman Mathew 4766, Janeth Mayanja kura 850, Rukia Mandindi kura 550, Ismail Mbani kura 419, Malick Mussa kura 173.


16. Mtwara


Mtwara Vijijini
Hawa Ghasia amepita bila kupingwa katika jimbo lake hilo.


Newala Mjini
George Mkuchika aliibuka mshindi kwa kubeba kura 5,826, Rajab Kazibure kura 3,247 na Kwame Daffari aliyepata kura 1,617


Nanyumbu
Abdallah Chikota alipata kura 12,388, Swalehe Livanga kura 2,376


Masasi 
Mkata Joseph kura 100, Mande Mike kura 186, Frank Ekoni kura 353, Mnonjela Joshua kura 441, Kombani Regnald kura 533, Mtaki Magreth kura 1,386, Mwambe Jofrey kura 1,787 na Chua Chua Rashid kura 2,412.


Lulindi
Halinga Richard Enock kura 896, Sowani Thomas kura 1,048, na Bwanausi Jerome kura 11,745.


Ndanda
Mrope Regnald kura 863, Mwambe Cecil kura 4,951 na Mariam Kasembe kura 5,453.


Mtwara Mjini
Hasnein Murji kura aliibuka kidedea kwa kura 10,055 Hussein Kasugulu kura 791, Said Swala kura 393, Mussa Mohamed Chimae kura 217, , Salum Nahodha 114


17. Tanga


Muheza
Adadi Rajabu ameibuka kidedea kwa kupata kura 7,101, Grace Mtunguja kura 5,033, Alan Muhina 3,002, Harbati Mtangi kura 2,502, Nicholas Mgaya kura 692, Laick Gugu kura 1,165, Hassan Bomboka kura 1,181, Julius Semwaiko kura 1,103, Mussa Kopwe kura 545, Omary Mhando kura 2036, Issa Msumari kura 624, Rajab Nkalange kura 262 na John Kwinga kura.


Bumbuli
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba alifanikiwa kutetea nafasi yake.


Korogwe Mjini
Mary Chatanda, alifanikiwa kuongoza katika jimbo hilo.


Korogwe Vijijini
Stephen Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu, alikuwa akiongoza katika jimbo lake, akifuatiwa na Dk. Edmund Mndolwa.


18. Dar es Salaam


Kinondoni
Mbunge anayemaliza muda wake, Idd Azzan ameibuka mshindi na kuwabwaga wagombea wengine, akiwemo aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Tanzania (FAT), sasa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Katibu Mkuu wa klabu ya Simba, Michael Wambura.


Ukonga
Jerry Silaa, amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika kinyang’anyiro hicho katika Jimbo la Ukonga.


Segerea
Jimbo la Segerea limanyakuliwa na Bona Kalua, kwa kumbwaga Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga, ambaye baada ya kushindwa akaamua kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


Kibamba
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara, amefanikiwa kushinda kura za maoni katika Jimbo jipya la Kibamba.

No comments: