Sunday, August 16, 2015

NAIBU KATIBU WA MADEREVA AZUNGUMZIA MGOMO WAO UNAOPANGWA KUANZA KESHO

Leo  Agosti 16 mwaka 2015 kulikuwa na mkutano wa madereva wa mabasi ulifanyika katika ukumbi wa Kimara resort jijini Dar es salaam na kuahamua haya yafuatayo;
Kwa mujibu wa Naibu katibu mkuu wa madereva (TADU), Rashidi Saleh aliwaeleza madereva hatima ya kamati ambayo imeundwa na Waziri Mkuu kusuruhisha kero za Madereva  hapa nchini.
Naibu katibu mkuu wa madereva (TADU), Rashidi Saleh akizungumza na madereva amesema "Tarehe 13 /8 tulipo kwenda baada ya wao kusikia kuna tishio la mgomo,tulizani kwamba tunakwenda kujadili kwanini tunataka kugoma kwasababu tunazo kero zetu matokeo tulikutana na ajenda ya mizani ya vigwaza ,tukakutana na matatizo ya wamiliki, kamati kwenda Zambia kwenye ukaguzi wa mafuta, kamati kukagua spidi za magari na timetable ya Sumatra wiki ijayo.Naibu Katibu TADU"
Pia alisema "Siku ya kesho Jumatatu Agosti 16 tutatoa tamko kwa waandishi wa habari kuhusu hatima ya madereva wa Tanzania, vyombo vyote vya habari kuanzia TV, Radio, Magazeti vitaonyesha kwahiyo kaeni karibu na vyombo vya habari"
 Amemalizia kwa kusema "Kuacha kuendesha sio mgomo si umepumzika,Nani kasema mgomo sisi  atugomagi uwa tunajipa likizo vibarua uwa analikizo yake mwenyewe mpaka sasa sisi bado  ni vibarua. Sisi tunataka  tuweke semina atakama ya siku tatu maana na sisi tunahasira na ajali hivyo tutawaita walimu waje watufundishe na wale ambao wapo Tunduma nao wasivuke kwasababu awatapata mafunzo maana redio haziskiki nje ya nchi"

No comments: