Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akizungumza ngumza na waandishi wa habari kuhusiana na kung'atua rasmi umwenyekiti wa chama hicho na kuendelea kuwa mwanachama wakawaida wa chama hicho ikiwa atakuwa mwanachama halali kwani kadi yake ya uanachama ameshailipia mpaka mwaka 2020 hayo ameyasema katika ukumbi wa mikutano wa Peacock hoteli jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akiwa na wananchi wa kawaida kulia, Abdala Shabani pamoja na mdogo wake,Shabaani Miraji wakiwa wamemsindikiza aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF taifa ili kuzungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya wananchi katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Iblahimu Lipumba akitanga kujihuzuru wadhifa wake katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Rasmu ya Katiba pendekezwa ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuwa ndio iliyosababisha kuungana na kuunda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akionyesha Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ambayo katika mkutano wa kujivua uenyekiti wa chama cha CUF leo jijini Dar es Salaam.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba akikusanya makabrasha yake mara baada ya kumaliza mkutano wa kujivua uanachama wa chama cha CUF taifa katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.
3 comments:
Lakini hajatoka CUF
Wala UKAWA
Lakini kuna chama kimeyavaliya njuga haya
Kama wanafikiri wanajuwa propaganda hats tunajuwa
October Jeuri yao na prof Lipumba tunaye
Ukawa mlimpokea FISADI kuwa mgombea wenu wa Urais. Do you see what you are getting now? Viongozi wenu wanaanguka one by one. Dr. Slaa is out and so is Prof. Lipumba. Sasa mtakuwa na viongozi gani? Wahuni na Mafisadi waliotoka CCM ndo wanabomoa Ukawa yenu. Jee? hiyo ndiyo safari yenu ya matumaini?
Wewe kama hujui siasa na diplomasia yake ulie tu. Prof. kwa kusema anajivua madaraka makubwa ya kukiendesha chama na kubakia mwanachama wa kawaida tu ni kutotaka kueleweka vibaya. Ukweli ni kuwa amafikia mwisho wa uvumilivu wake kutokana na maamuzi yasiyo ya kidemokrasia yanayofanywa na baadhi ya viongozi katika mshikamano wa Ukawa. Mtu akikuambia kuwa alikuwa anapigania katiba mya ya nchi na haikupitishwa na kati ya wale walioipinga ndiyo anakuja kwenu na kupewa nafasi ya kuwa mgombea pekee wa urais ujue kuwa kuna kasoro hapo. Kama hiyo katiba aliikataa huko alikotoka ni jambo gani litakalomfanya leo abadilishe msimamo wake huo na ni nani atakayethubutu kumtaka abadilike. Ujue kabisa kuwa hao waliompokea wanafahamu fika msimamo wake na huenda wako naye katika mismamo huo. Wewe na mimi ambao wala hatukukarishwa ktuoa maoni yetu ya kumpokea na hatimaye kumteua kuwa mgombea pekee wa urais tutathubutu kusema lolote? Kaa chonjo, siyo mtu anathaminika hapa bali ni mali tu. Kama una hela utasikilizwa hata ukiwa fisadi buku. Kama huna basi ulie tu.
Post a Comment