ANGALIA LIVE NEWS

Friday, August 7, 2015

TAMASHA LA UHAMASISHAJI WA KUSOMA VITABU LAFANYIKA MICHEWENI

 MSAIDIZI Mkutubi Mkuu wa Shirika la Huduma za Maktaba Zanzibar, Abdalla Omar akielezea namna ya uzinduzi wa tamasha la uhamasishaji wa kusoma vitabu, kwa wanafunzi na wananchi wa wilaya ya Micheweni Pemba, lililofanyika juzi.
 AFISA Elimu na Mafunzo ya Amali wilaya ya Micheweni Pemba Mbwana Shaame, akielezea faraja yao, kwa Shirika la Huduma za Maktaba Zanzibar, tawi la Pemba kuanza wilaya hiyo, uzinduzi wa tamasha la uhamasishaji wa usomaji wa vitabu kwa wananchi na wanafunzi lililofanyika skuli ya Micheweni.
 AFISA Uendeshaji kutoka wizara ya elimu na mafunzo ya amali Pemba, Salim Ali Mata, akisoma hutuba kwenye uzinduzi wa tamasha la uhamasishaji wa usomaji wa vitabu, lililoandaliwa na Shirika la Huduma za Maktaba Pemba na kufanyika skuli ya Micheweni.
 BAADHI ya vitabu vilivyotayarishwa na Shirika la Maktaba Zanzibar kisiwani Pemba, kwa ajili ya kusomwa na wananchi na wanafunzi wa wilaya ya Micheweni, kwenye tamasha la uhamasishaji wa usomaji wa vitabu hivyo lililodumu kwa muda wa siku mbili.

 AFISA Uendeshaji kutoka wizara ya elimu na mafunzo ya amali Pemba, Salim Ali Mata, (kushoto) akionyeshwa baadhi ya vitabu vilivyotayarishwa na Shirika la Maktaba Pemba na Msaidizi Mkutubi Mkuu Abdalla Omar, kwenye tamasha la uhamasishaji wa kusoma vitabu lililofanyika skuli ya Micheweni Pemba.
BAADHI ya wanafunzi wa skuli za sekondari za wilaya ya Micheweni wakisoma na wengine kuchagua vitabu, kwenye tamasha la uhamasishaji wa usomaji wa vitabu lililoandaliwa na Shirika la Maktaba Pemba na kufanyika skuli ya Micheweni, (Picha na Haji Nassor, Pemba).    

No comments: