ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 17, 2015

Kutana na mbuzi apendaye chai Somalia


Image copyrightMohamed JabraImage captionMbuzi huyo aliinywa chai hiyo upesi ingawa ilikuwa moto
Kwa wale wapendao sana kunywa chai, kuna mbuzi ambaye ameonyesha kila sifa za kutoa ushindani mkubwa kwao.
Mohamed Jabra, mpiga picha eneo la Gaalkayo, katika jimbo la Puntland, kaskazini mashariki anasema baada ya kula chakula cha jioni jana alienda mkahawani akiwa na rafiki yake na akaagiza vikombe viwili vya chai.

“Ghafla mbuzi ailikuja na akajaribu kunywa chai yangu,” aliambia BBC.

"Nilijaribu kumzuia lakini aliinywa haraka na nililazimika kumuacha aimalize.”

Anasema mbuzi huyo alibugia chai hiyo upesi ingawa ilikuwa moto.Image copyrightMohamed JabraImage captionMaziwa ya mbuzi wakati mwingine hutumiwa kwenye chai

“Nililazimika kujituliza kwa kujiambia kuwa chai hiyo ilikuwa na maziwa ya mbuzi, hivyo basi mbuzi huyo alikuwa na haki kuinywa.”

No comments: