ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 17, 2015

NCCR-MAGEUZI LEO IMEJIONDOA RASMI "UKAWA"


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-MAGEUZI, Reticia Ghati Mosore akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari katika Hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam muda huu kuhusiana na ukiukwaji wa taratibu katika umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) na kutangaza kuendelea na mapambano nje ya umoja huo wa vyama pinzani. 
Katibu Mkuu wa NCCR-MAGEUZI, Mosena Nyambabe akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatima yao ya kupambana kama wenyewe NCCR-MAGEUZI bila ya UKAWA na kuwa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuwa inavibana vyama vishiriki vya UKAWA katika maamuzi.

8 comments:

Anonymous said...

Kazi ipo mwaka huu
Kila kona

Anonymous said...

wameshapewa posho...not surprised na ndiyo maana hatu move forward.....

Anonymous said...

Mna tuchanganya tu sisi waouga kura sasa na nyie NCSR mmetumwa na CCM?

Anonymous said...

je maamuzi haya ni chama au ni viongozi tu wameamua, mbatia mumeitisha vikao vya chama kwa maauzi haya, au mshachukua chenu mnakaa pambeni kama akina slaa na lipumba

Anonymous said...

Vipi position ya Mbatia ambae amejibatiza kuwa msemaji mkuu wa Lowasa?

Anonymous said...

Watanzania tuwe na uoga wa kumugopa mungu kila mtu akitoa mawazo yake kesha nunuliwa,hivi watu wote wanatakiwa kuwa ukawa kwa kuwa ninyi ni malaika??Hata kama watu wanaburuzwa wabaki kupiga makofi na kushangilia,Maana ya Demokrasia ni uhuru kamili wa mtu au watu kutoa mitizamo yao kwa uhuru kamili na si huu muelekeo mlio nao ninyi wa kila mwenye mawazo mbadala kanunuliwa lakini sishangai kwa hayo ndo matunda ya uongo wa watu wanaojidai kuamini na kunadi yale wasiyofuata kiuhalisia

Unknown said...

Ushuzi mtupu kila kitu CCM, Dk slaa kaingia mitini kwa sababu ya ukiukwaji wa misingi walio jiwekea wao wenyewe hasa baada ya akina Mbowe kurubuniwa na mzee lowasa haikuchukuwa muda haraka haraka wanakimbilia kusema kanunuliwa na CCM, Lipumba nae kanunuliwa na CCM, Zito nae kanunuliwa na CCM, NCCR MAGEUZI baada ya kushtuka na kuona wanapoelekea pabaya na kuamua kujiondoa ukawa na wao vile vile wamenunuliwa na CCM halafu mkiambiwa wapumbavu na malofa mnan'gaka Aaagh! tunatukanwa hamtukanwi bali mnajitukanisha kwa kukumbatia fikra hewa na kuacha kuikubali hali halisi ya mabo ilivyo. Hali halisi yenyewe ni hivi mtanzania popote ulipo kama America, Asia ,EUROPE na kwenguneko Duniani fahamu kuwa kama Lowasa na ukawa wana nafasi ya kushinda Uraisi mwaka huu basi NCCR MAGEUZI wasingetangaza kujiondoa ukawa katikati ya kampeni kwa sababu waponyumbani kwenye uwanja wa mapambano wanashuhudia kinachoendelea na bila shaka kutokana na hali halisi wameshajionea hata hizo nafasi za ubunge walizokuwanazo bungeni itakuwa tabu saba kuzipata tena . Kumbuka NCCR MAGEUZI ni washirika wa serikali ya ukawa kama watafanikiwa kushinda uraisi kwa hivyo katika makubaliano yao wana baadhi ya nafasi za mawaziri wa nchi lakini wameshaona hizo sasa ni ndoto tena za mchana.

Anonymous said...

Ni kweli hawa wameshachukua chao! wasitake kukatisha tamaa Watanzania.
Haturudi nyuma hapa ni mbele kwa mbele, mafuriko hayasubiri tone