Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akinadi sera zake kwa umati wa wakazi wa Mji wa Dodoma waliokuwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini humo leo Septemba 11, 2015, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Mikutano yake ya Kampeni za Uchaguzi Mkuu, unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.PICHA NA OTHMAN MICHUZI, DODOMA
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi Mgombea wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Benson Kigaila, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma leo Septemba 11, 2015.
Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye, akiwahutubia wananchi wa mji wa Dodoma waliofurika kwa wingi wao kwenye Uwanja wa Barafu mjini humo, kwa ajili ya kusikiliza sera za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa.
Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu akiwaga cheche zake katika Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma.
Shangwe za nguvu wakati Chopa ya Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, ikiwasili uwanjani hapo.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, alieambatana na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye, wakiwasili kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwa kwenye gari lake la wazi huku umati wa wananchi wa Dodoma ukimsindikiza wakati akitokea kwenye Mkutano wa Kampeni uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Barafu, Mjini Dodoma leo Septemba 11, 2015.
12 comments:
This is an election that will surely lay to rest the political careers of these thugs (Lowasa and Sumaye)!
Tena ni ubora ulitukuka,anonymous wa kwanza u just bitter person,get life
This is an election that the world will see how wise full and strong Tanzanian's have become to put this thug CCM into the grave..death to CCM !! Uncle please don't trash my comments. .
Mtasema sana but Lowassa it's our choice no way
Wakati ni busara kuheshimu maoni ya mtu yoyote, ila nashangazwa sana na baadhi ya maudhui ya wachangiaji humu. Mfano, mchangiaji wa awali kabisa kwa kweli anasikitisha sana, alicho andika kinaonyesha zaidi chuki zake binafsi tu kwa EL, na kwa hilo anawajumuisha wote wanaoshiriki kumuunga mkono. Kama event ya EL hapo Idodomya haikukufurahisha haukuwa na ulazima wa kutoa maoni. Wakati mwingine kukaa kimya huwa ni bora zaidi ya kuongea/ kuandika kitu kinachoonyesha upungufu mkubwa wa mchangia mawazo.
Should EL took power after October 25, I guess most of hater's like the first commentator will get hypertension.
Poleni sana
Ubora gani aliokuwa nao huko dodoma wakati lowasa alipowakaribisha wananchi kumuliza maswali alitokea mwananchi wa kawaida tu aliemtaka Edwadi lowasa amjibu kuhusu kashfa la Richmond kama alihusika au la ? Jibu la lowasa kwa mwananchi huyo lilikuwa hilo suala la Richmond halina maana. Kweli suala Richmond halina maana kufafanuliwa kwa wananchi kutoka kwa mtuhumiwa mkuu? Suala jengine kutoka kwa wananchi hao kwa lowasa lilikuwa kama alishindwa kudhibiti mapambano kati ya wachungaji wa mifugo ya kimasai na wakulima katika maeneo anayoyaongoza kama mbunge kwa miaka yote hiyo vipi ataweza kutatua migogoro ya ardhi inayoikabili nchi? Vile vile mzee lowasa kashundwa kujibu suala hilo kasema hilo suala halina maana. Kweli migogoro ya ardhi haina maana kutafutiwa ufumbuzi? Hapa hapana kiongozi maagizo tu.
Huge crowds followed and attended one presidential candidate's meetings in 1995 but the candidate lost. It's gonna be same again this year.
CCM will survive and witness the demise of UKAWA
Mimi nawashangaa wasanii wanaoshabikia CCM kama kweli wana akili timamu au wamerogwa? CCM have done nothing kuendeleza nchi zaidi ya kuiba na kuleta usanii kama wasanii wenyewe. Mpaka leo Tanzania tuna matatizo yale yale toka mwaka tumepata uhuru, hakuna maji, umeme, hospitali hakuna dawa, na barabara ndiyo usiseme ni maandaki tu. In short, viongozi wa CCM ni wale wale wana akili ya mgando na si wapenda maendeleo. Lazima hiki chama kife tu mwaka huu na viongozi wao wakamatwe kwa wizi wao.
Endelea na ndoto zako Oktoba 25, 2015 utaiona Ikulu ukipita pembeni kama mtalii. CCM Oyeeeee!
Andika Kiswahili ndugu yangu ueleweke; EITHER your English teacher shirked his or her responsibilities OR you chronically skipped your English classes!
Nadhani utimamu wa akili yako wewe ndio unahitaji kuchunguzwa. Kwanini usijishangae wewe unayeshabikia rejects wa CCM? Kumbuka, hao walikuwa makada wa CCM wa miaka nenda rudi na ndio waliohusika kuifikisha CCM hapo ilipo na hawakuhama CCM kwa sababu ya ubaya wa CCM bali walifanya hivyo baada ya kukosa ridhaa ya wana CCM!
Post a Comment