ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 6, 2016

MWAMBATA WA ZAMANI WA JESHI UBALOZI WATANZANIA NCHINI MAREKANI NA CANADA BRIGADIEAR GENERAL EMMANUEL MAGANGA ASTAAFU RASMI

\
Mwambata jeshi wa zamani nchini Marekani na Canada Brigadier General Emmanuel Edward Maganga siku ya ijumaa trh 04 March alikuwa miongoni mwa majenerali 16 walioagwa rasmi baada ya kustaafu utumishi jeshini. Jenerali Maganga amestaafu akiwa na wadhifa wa Mkaguzi Mkuu wa Jeshi. Amelitumikia jeshi kwa takriban miaka 37 na mwezi mmoja. Katika utumishi wake zaidi ya kuwa Mwambata jeshi USA na Canada pia aliwahi kuwa Mwambata Jeshi nchini Africa ya Kusini akiwa pia analiwakilisha jeshi katika nchi za Angola, Botswana,Lesotho na Namibia. Watanzania walioko Marekani watakumbuka upendo wake kwao akiwa na mke wake Untie Love na ushiriki wao usiobagua katika matukio ya raha na shida. Timu ya VIJIMAMBO inamuombea maisha mapya ya furaha na kumkaribisha URAIANI. Hongera SANA Kamanda, mwanataaluma ya uandishi wa habari, mwanadiplomasia, mwanamikakati, Mkaguzi uliyebobea na mwanamichezo madhubuti.

1 comment:

African Queen said...

Naam
Nasi watanzania tulioko nyumbani Tunampongeza, na tunamkumbuka Brigadier General Maganga kwa upendo, ucheshi wake yeye na mke wake Love, upendo usiobagua raha wala shida, tajiri wala maskini. Binafsi lift za hapa na pale walizonipa nikiwa ughaibuni – Marekani, nazo nazithamini. kama Mzee wa Kanisa namwombea Baraka na kheri siku zote! Karibu uraiani, karibu kwenye diplomasia.

Kila la kheri