ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 15, 2016

MSIBA WASHINGTON D. C.: BABY ESTHER NNKO FUNERAL UPDATE

MSIBA DMV

Mtoto Esther akiwa na wazazi kipindi cha uhai wake

Tunapenda kutoa taarifa kuwa tumefanikiwa kutimiza lengo la kupata fedha zote za gharama ya mazishi ya mtoto Esther (1 year old).  Tumefanya malipo yote leo Alhamis.  Familia ya Nnko inatoa shukrani kwa wote walio wezesha kufanikisha lengo hili.  Mungu awazidishie.

Pia tunapenda kuwajurisha kuwa, mazishi ya mtoto Esther yatafanyika Jumatano, April 20, 2016, kuanzia saa Sita mchana (12:00pm) kwenye makaburi ya Fort Lincoln. 

Misa na heshima ya mwisho kwa marehemu itaanza saa Sita mchana (12:00 pm) hadi saa Saba mchana (1:30 pm).  Baada ya misa, tutafanya mazishi na kurudi ukumbini kusherehekea maisha ya mtoto Esther hapo hapo Fort Lincoln.

Anuani ya sehemu ya mazishi:
3401 Bladensburg Road,
Brentwood, MD 20722

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Peace Kachuchuru 301 367 6378
Jessica Mshara  301 807 4934

BWANA AMETOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIDIMIWE.

No comments: