Advertisements

Tuesday, April 5, 2016

MWENYEKITI WA CHADEMA IRINGA VIJIJINI APATA AJALI NA KUFARIKI

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wa Wilaya ya Iringa Vijijini Sinkala Mwenda amepata ajali jioni ya leo eneo la Tanangozi. Amekimbizwa hospitali lakini kafariki dunia usiku huu.

Sinkala Mwenda alikua Mwanasheria Kijana Msomi wa CHADEMA. Mwenda alikuwa mgombea kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi mdogo wa Jimbo la Kalenga 2014 ambaye aliwashinda wagombea wengine 12 katika kura za maoni ndani ya chama, alipokwa ushindi na chama hicho na kikamteua mshindi wa pili Grace Tendega kupeperusha bendera katika uchaguzi mdogo huo.
Wakati wa uhai wake alikuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Iringa Vijijini

No comments: