Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na kusainiwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja inaeleza kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kujionea maendeleo ya mradi wa mabwawa ya samaki yaliyopo gerezani hapo ambayo hadi sasa yamepandwa vifaranga wa samaki 18,800 tangu tarehe 16/12/2015.
Kabla ya kutembelea eneo la mradi wa mabwawa ya samaki, Naibu Waziri, Mhe. Ole Nasha atapokea taarifa fupi ya maendeleo ya mradi wa uzalishaji samaki Gereza Kwamugumi, Korogwe.
Miradi ya ufugaji samaki ipo katika Magereza ya Karanga, Njombe, Masasi, Tukuyu ambapo nia ya Uongozi wa Jeshi la Magereza ni kuieneza katika Magereza mbalimbali yenye fursa za kuendesha mradi huo.
Mradi wa uzalishaji samaki katika Gereza Kwamugumi ni mojawapo ya miradi mbalimbali ya uzalishaji mali iliyoanzishwa na Uongozi wa Jeshi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazolikabili Jeshi la Magereza, hususan katika kuipunguzia Serikali gharama za kuhudumia Magereza na kuongeza pato la kodi kwa Taifa.
Imetolewa na Lucas Mboje, Mrakibu Msaidizi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
DAR ES SALAAM
14 Aprili, 2016
No comments:
Post a Comment