Papa Francis leo amewakaribisha wakimbizi 12 wa
Syria wakati wakiwasili Jijini Roma baada ya kuwachukua kutoka kwenye
kambi ya Lesbos kufuatia ziara yake katika kisiwa hicho cha Ugiriki.
Familia tatu za wakimbizi wa Syria walipanda ndege
ya Papa Francis punde tu baada ya ziara yake hiyo ya Lesbos kuangazia
mgogoro wa kibinadamu unaotokana na wakimbizi.
Papa Francis akiwakaribisha wakimbizi wa Syria aliowachukua Lesbos
Msemaji wa Vatican amesema Papa Francis ameamua kuonyesha ishara ya kuwakaribisha wakimbizi hao kwa kuwachukua kukaa Roma ambao miongoni mwao wamo watoto sita.
Papa Francis akimbusu mtoto mkimbizi wakati wa ziara yake ya Lesbos
Papa Francis akisalimiana na wakimbizi waliopo Lesbos Ugiriki
1 comment:
Siasa zote hizi. Mbona hajachukua wakimbizi wa Butundi?
Post a Comment