Familia ya Emmanuel na
Hawarita Nnko tunatoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa na marafiki wote walio
tusaidia kufanikisha mazishi ya mtoto wetu Esther Nnko. Kwa msaada wenu wa hali na mali tumefanikiwa
kumpumzisha mtoto wetu Esther jana, Jumatano, April 20, 2016 kwenye makaburi ya
Fort Lincoln.
Mtoto wetu Esther alizaliwa
March 21, 2015 na kufariki April 9, 2016.
Tunawashukuru wote kwa moyo wa upendo, ushirikiano na msaada mlio
uonyesha kwenye kipindi hiki kigumu cha kumpoteza mtoto wetu. Hatuna cha
kuwalipa kwa fadhira zenu bali tunaomba mnyezi Mungu aendelee kuwabariki,
kuwalinda na kuwaendelezea upendo mlio onyesha
BWANA AMETOA: BWANA AMETWAA,
JINA LAKE LIHIMIDIWE
The Nnko Family
No comments:
Post a Comment