Kuhusu Ajali ya Tundamani aliyepata ajali ni Promota
na amefariki Dunia na ndo alikuwa anatumia gari ya Toyota aina ya Avalon na
Tundaman na wenzake walikuwa kwenye Noah na huyo promota ndo alikuwa
ametangulia kwenye msafara.Ajali hiyo imetokea Eneo la Idetelo,
katikati ya Nyololo la Makambako. Promota huyo amefariki kwenye gari aina ya
Toyota Avalon. Maiti inapelekwa hospitali ya wilaya ya Mufindi ni kwa
mujibu wa Dj Nas aliyekuwa kwenye gari na Tundaman.
Maelezo ya mwanzo ya Tunda Man amesema ‘Tulikua
tunatoka Njombe baada ya kumaliza show yetu na tukasema bora tusilale tuwahi
kufika Dar,tumetoka Njombe saa 10 alfajiri mimi nikawa nasikia usingizi
nikamwambia mwanangu hebu tuendeshe kidogo,kufika kijiji cha Idetelo kilomita
kama 20 au 30 kabla ya kufika Mafinga tukiwa tumelala tukashtuka Gari inaingia
porini tukasikia mshindo mkubwa gari imepiga puuuh Dereva hapo hapo akawa
amefariki‘
Tunda Man anamalizia kwa kusema ‘Tulikua watu
watano kwenye gari aliyekaa mbele na Dereva amevunjika mkono na nyama
zimechanika,kuna mtu aliyekua nyuma mapafu yamepasuka,Mimi nipo poa,kwa sasa
hivi tuko Mafinga hapa Hospitali ya Wilaya tunaangalia taratibu za kuchukua
mwili tuupeleke Kilosa kwa ndugu zake,marehemu aliyefariki anaitwa Mussa lakini
watu wengi wanamjua kwa jina la Man katuzo.
No comments:
Post a Comment