Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Jenista Mhagama,akizungumza katika katika uzinduzi wa matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014. Uzinduzi huo ulifanyika katika Viwanja vya Karimjee,Dar es Salaam, jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo na Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu nchini,Dk.Albina Chuwa.
Na Al-Hassan Michuzi.
Serikali imezindua utafiti wa Ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu, (NBS) ya Watu wenye uwezo wa kufanya kazi leo jijini Dar Es Salaam ,katika uzinduzi huo imeelezwa kuwa utafiti huo utasaidia kufuatilia na kutathmini katika kufanya mipango ya maendeleo.
Akizungumza katika Uzinduzi wa Ripoti ya Utafiti wa Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi uliofanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Uratibu wa Bunge,Kazi, Walemavu, Jenister Mhagama, amesema kuwa matokeo ya utafiti yatasaidia kupata ufahamu wa hali halisi ya soko la ajira katika kuingia katika uchumi wa pato la kati 2020-2025.
Waziri Jenister amesema kuwa utafiti huo utasaidia kutengeneza Sera,mpango wa kupambana na kupunguza Umasikini nchini (Mkukuta) na mpango wa maendeleo wa miaka mitano katika kupata suluhisho la tatizo la ajira.
Amesema nguvu kazi ya vijana kati ya miaka 15 hadi 35 sawa na milioni 15.1 na asilimia 68, hivyo utafiti huo utatibu swali vijana la ukosefu wa ajira.Jenister amesema fursa zitakazotolewa ziweze kutatua changamoto zilizopo kwa vijana na lazima zitoe tija, na Tanzania kuwa ya kwanza duniani katika uongezaji wa ajira kutokana fursa ambazo serikali itatekeleza.
Amesema sekta ya kilimo ndio inaweza ikifanya vizuri katika kutoa ajira kwa vijana kama sekta kiongozi.Amesema asilimia 35 ya sekta binafsi ndio yenye ajira kubwa kuliko ya sekta ya umma hivyo utafiti lazima utumike katika kufanya mipango.Kiwango cha upungufu wa ajira kwa wanaume ni asilimia 8.4 na wanawake ni asilimia 12.4 hivyo ukosefu wa ajira kwa wanawake uko juu kuliko wanaume..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu),Jenista Mhagama,akionesha ripoti ya matokeo ya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi wa mwaka 2014 katika Viwanja vya Karimjee,Dar es Salaam. Wengine wanaoshuhudia ni kushoto kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Takwimu nchini,Dk.Albina Chuwa, Mkurugenzi wa Sensa ya watu na Takwimu za Jamii,Ephraim Kwesigabo na Mwakilishi kutoka Shirika la Kazi Duniani,Marry Kawar.
No comments:
Post a Comment