ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 15, 2016

WABUNGE WAPONGEZA KUANZISHWA KWA TADB

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Florens Turuka (Kulia) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo naviongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TADB, Dkt. Anaclet Kashuriza (Aliyesimama) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakifurahia jambo wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.

Na Mwandishi wetu

Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Kilimo, Mifugo na Maji imeipongeza Serikali kwa kuanzisha kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) yenye lengo la Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania na kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini.

Wakizungumza na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB wakati wa vikao vya kamati za Bunge vinavyoendelea jijini Dar es Salaam. Wabunge hao wamesema kuwa TADB imekuja wakati muafaka kwa kuwa itachagiza juhudi za kuinua na ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini nchini Tanzania.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Mary Nagu amesema kuwa licha ya umuhimu wa Sekta ya Kilimo, bado ukuaji wa sekta hiyo ulikuwa ukikabiliwa na changamoto mbali mbali kuu ikiwa ni Ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini.

“Kwa kweli tunapongeza kwa kuanzishwa Benki hii kwa kuwa kwa miaka mingi mikopo mingi kutoka taasisi za fedha imekuwa ikielekezwa zaidi kwenye upande wa biashara za bidhaa na kuwa na riba kubwa kwenye mikopo ya kilimo,” alisema Mhe. Nagu.

Wabunge hao wametoa wito kwa Serikali kuiongezea mtaji Bnki hiyo ili kuongeza kasi ya utendaji kazi wa Benki hiyo.

Akizungumza kwenye kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Florens Turuka alisema kuwa TADB inajihusisha na aina zote za kilimo kwa ule wigo mpana wa maana ya kilimo, ambao inahusisha mazao, ufugaji, uvuvi, na bidhaa zitokanazo na misitu. Na kuongeza kuwa katika kusaidia minyororo ya thamani ya mazao ya kilimo, TADB itakuwa inatoa fedha kwenye hatua mbali mbali za Uzalishaji na uongezaji wa thamani kama vile Uzalishaji wa awali; uhifadhi; usindikaji; uchakataji; usafirishaji; na masoko.

“Uanzishwaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Nchini kama taasisi ya maendeleo ya fedha, kulitokana na Wizara yangu, na baadaye mawazo ya Wadau mbalimbali chini ya uratibu wa Baraza la Taifa la Biashara kuhusu jinsi Tanzania inavyoweza kufikia mapinduzi ya kilimo,” aliongeza Dkt. Turuka.

Kwa mujibu wa Dkt. Turuka, katika maazimio kumi (10) ya Kilimo Kwanza yaliyofikiwa mwaka 2009, azimio la tatu lilikuwa kuanzishwa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo. Hivyo uanzishwaji wa benki hii ni muendelezo wa Serikali katika kutimiza na kutekeleza maazimio ya “KILIMO KWANZA”. Hii ilitokana hasa na kuwepo kwa changamoto mbali mbali kwenye Sekta ya Kilimo ikiwemo upatikanaji wa fedha na mikopo ya riba nafuu katika kuendeleza sekta ya kilimo nchini kwa miradi mikubwa ya kilimo, ya kati na midogo inayolenga kuimarisha minyororo ya thamani ya Kilimo.

Naye Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi alisema kuwa kama yalivyo matarajio ya Serikali, kuanzishwa na kuanza kufanya kazi kwa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Nchini, kunategemewa kuwa na umuhimu wa kusaidia upatikanaji wa mali ghafi kwa viwanda vya ndani hivyo kusukuma ndoto ya Serikali kufikia lengo lake la Kujenga Uchumi wa Viwanda.

Ameongeza pia TADB inatarajia kuhuisha uwekezaji kwenye Viwanda vidogo vidogo na vya kati vya usindikaji na uchakataji wa mazao ya Kilimo na mifugo pamoja na kuboresha kwa upatikanaji wa mikopo na huduma za kifedha kwenye miradi ya maendeleo ya Kilimo kwa riba nafuu zilizo chini ya viwango vya kibiashara kwenye soko.

Benki ya TADB ni mali ya Serikali kwa Asilimia 100 ya Hisa na kwa kuzingatia muundo wa uendeshaji wa shughuli za Serikali hususan kwenye masuala ya kifedha, Benki ya Maendeleo ya Kilimo iko chini ya Wizara ya Fedha na Mipango. Hali kadhalika, benki iko chini ya Uangalizi wa Msajili wa Hazina kama yalivyo mashirika mengine ya Umma. Hata hivyo, kiutekelezaji, TADB inajihusisha moja kwa moja na Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, kwani muktadha wa uanzishwaji wake umelenga moja kwa moja kwenye Sekta ya Kilimo kuliko Sekta nyingine yoyote.
 Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi (Kulia) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Katikati) akifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB (hayupo pichani) wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
 Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi (Kulia) akizungumza mbele ya Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. Dkt. Mary Nagu (Kulia) akitoa maelekezo kwa viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB wakati walipokutana na Kamati yake.
 Viongozi wa Waandamizi wa TADB wakifuatilia kwa makini maelekezo ya Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
 Baadhi ya Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wakitoa michango yao wakati wa kikao cha pamoja kati ya Kamati hiyo na viongozi kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na menejimenti ya TADB.

No comments: