Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe wakati alipokwenda kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na mwanasiasa mkongwe,Kingunge Ngombale- Mwiru wakati alipokwenda kumpa pole Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha kaka yake Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe (kulia kwake) wakati alipokwenda kumpa pole kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana akisalimiana na wanafamilia wakati alipokwenda kumpa pole Mwenyekiti wa CHADEMA na kiongozi wa Upinzani Bunge, Freeman Mbowe kufuatia kifo cha kaka yake, Kanali Mstaafu Maximillian Aikaeli Mbowe, nyumbani kwa marehemu, Tegeta jijini Dar es salaam Aprili 16, 2016.
2 comments:
Babu Kingunge bado yupo mjini? Mie ningetoroka!
Kwa nini unafikiri kuwa Kingunge hana haki ya kuwepo mjini? Angetoroka kwa kosa lipi alilolifanya? au kuwa mrengo wa mawazo mbadala kiitikadi (ideology) na mfumo uliopo madarakani (wa Ki- CCM) na kuamua kutoka ndani ya mfumo huo basi ndio kishakuwa criminal?
Hayo ni mawazo mgando ndugu yangu kwani Tanzania ni ya watu wote. Kila mtu ana haki ya kuishi jinsi anavyopenda na kuamini mfumo wa Chama au itikadi anayoiitaka. Na hakuna haja ya kuhukumiana kwani hakuna mwenye hati milki ya Tanzania isipokuwa WaTazania wote, kila mmoja wetu kwa haki yake mwenyewe. Period!
Post a Comment