Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman
akimuapisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kuwa mjumbe wa Baraza la
Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake kwenye
Baraza hilo huku Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akishuhudia tukio hilo katika Ikulu ndogo ya
Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akimpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein mara baada ya
kuapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri katika Ikulu ndogo
ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed
Shein, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa na Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman mara baada ya
tukio la uapisho. PICHA NA IKULU
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed
Shein leo asubuhi tarehe 02 Mei, 2016 ameapishwa kuwa mjumbe wa Baraza la
Mawaziri ili aweze kushiriki na kutekeleza majukumu yake ndani ya Baraza hilo.
Rais Shein ameapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mohamed
Chande Othman katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma, tukio
ambalo limeshuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli.
Viongozi wengine walioshuhudia tukio hilo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu
Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi.
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli leo mchana ameongoza kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika
katika ukumbi wa mikutano wa Baraza la Mawaziri, uliopo Ofisi ya Rais
TAMISEMI Mjini Dodoma.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dodoma
02 Mei, 2016
No comments:
Post a Comment