Meneja mradi wa VISTA Fred Grant akiongea kumkaribisha Mgeni Rasmi Mh Richard Kasesela
Sheikh Mwang'amilo akimpongeza Mkuu wa Wilaya na kuwaomba wananchi walime viazi vitamu kwa wingi na kuacha kunywa ovyo pombe.
Meneja Mkuu kiwanda cha Tosti ambao ndio wanunuzi wakubwa wa viazi akitoa melezo. Kiwanda hiki kipo Iringa na kina mahitaji ya viazi kiasi cha tani 150 kwa wiki za viazi mbalimbali.
Hafra hiyo iliyo andaliwa na mradi wa Viazi Lishe "Viable Sweet Potato Technlogies in Africa-VISTA na kufadhiriwa na seriakli ya watu wa Marekani (USAID) unajumuisha Halmashauri 7 ikiwemo IRinga, Wangingombe, Gairo, Mufindi, Ulanga,Mbozi na Chunya.
Katika mradi huo wakulima wanahamasishwa kulima viazi lishe kwa ajili ya afya ya mama na mtoto na pia kwa ajili ya biashara ambapo bidhaa kama juice, chapati, kakau(clips), tambi, mkate , maandazi na bidhaa zingine nyingi huweza kutengenezwa ili kukuza kipato.
Akimkaribisha mgeni rasmi Meneja wa Mradi wa VISTA Bwana Fred Grant alisema mradi huu uko katika mwaka wa 2 na ni wa miaka 3 ni muhimu Tanzania ikaanza kufikiria jinsi ya kuuendeleza nchi nzima kwani manufaa yake ni makubwa. Sherehe hizo pia zilihidhuriwa na waakilishi kutoka Halmashaurizote 7 zinazonufaika na mradi huo.
No comments:
Post a Comment