Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz akisaini mkataba wa kufanya kazi na msanii Rich Mavoko huku Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza akishuhudia tukio hilo. Nyuma ni uongozi wa WCB na msanii Diamond.
Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz akibadilishana mkataba na Rich Mavoko mara baada ya kusaini huku Katibu Mtendaji wa BASATA, Godfrey Mngereza akishuhudia tukio hilo.
MSANII wa Muziki wa Kizazi kipya, Diamond Platnumz amezindua rasmi Lebo ya muziki ‘WCB Record Label’ na kuwatangaza wasanii wanaosimamiwa na lebo hiyo huku msanii Rich Mavoko akisaini mkataba wa kufanya kazi na Lebo hiyo katika Hoteli ya Regency jijini Dar es Salaam.
WCB inakuwa ni lebo ya kwanza nchini Tanzania kuanzishwa na kusimamiwa na mwanamuziki, ikilinganishwa na lebo kadhaa ambazo zilikuwa zikisimamiwa na wadau waliokuwa katika tasnia ya sanaa na burudani.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu WCB, Diamond Platinumz alisema lengo la kuanzishwa lebo hiyo ni kusaidia vijana wenye vipaji na kuifanya sanaa ya muziki izalishe pato la taifa.
Msanii Diamond ameomba serikali kuwaunga mkono ili waweze kusonga mbele maana kwa sasa amekuwa na watu kadhaa ambao wamekuwa wakimtegemea katika kufanya sanaa ya muziki.
Chanzo: Michuzi Blog
No comments:
Post a Comment