Ulinzi wa polisi viwanja vya mahakama kuu kanda ya Iringa leo kabla ya mtuhumiwa wa mauwaji kufikishwa.
Wananchi wakiwa foleni kukaguliwa kabla ya kuingia mahakamani leo.
Mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi akipakiwa kwenye gari za FFU
Msafala wa gari za FFU zilizomsindikiza askari mwenzao anayekutwa na kosa la kuua bila kukusudia leo
Askari wa FFU wakitoka mbio mahakamani hapo
Wananchi na wanahabari wakitoka mahakamani hapo
Wakili
kutoka mtandao wa watetezi wa haki za
binadamu ((THRDC), Benedict Ishabakaki akizungumza na wanahabari nje ya viwanja vya mahakamani leo
Askari hao wakimtoa mahakamani hapo leo mtuhumiwa wa mauwaji ya Mwangosi
Na MatukiodaimaBlog Iringa
MAHAKAMA kuu kanda
ya Iringa imemtia hatiani kwa
kosa la kuua bila kukusudia
askari Polisi Kikosi cha Kutuliza
Ghasia ( FFU )Iringa G 58 Pacificius
Cleophace Simon (27) anayetuhumiwa kuuua
mwaahabari Daudi
Mwangosi mwaka 2012 katika kijiji
cha Nyololo wilaya ya
Mufindi.
Hata hivyo mahakamani
hiyo imesema adhabu
kwa mtuhumiwa huyo
kutokana na kupatikana na kosa
hilo la kuua bila kukusudia
itatolewa Julai 27 majira ya
saa 4 asubuhi mwaka
huu.
Jaji Dkt Paul Kiwelo ambaye anayesikiliza
kesi hiyo alisema mahakakamani hapo jana kuwa kati
ya vielelezo vitano vyote
vilivyoleta kama ushahidi
mahakamani hapo kwa ajili ya
kesi hiyo namba 54 ya
mwaka 2013 ni kielelezo
kimoja pekee cha
ungamo kwa mlinzi
wa amani ambacho ndicho
hakukuwa na shaka na ungamo
hilo ndilo lililomtia hatiani asikari
huyo.
Alivitaja vielelezo
vilivyopelekwa kama ushahidi kuwa ni Ramani ya
eneo la tukio,ripoti ya
tabibu ,ungamo la mlinzi wa amani ,silaha aliyoitumia
na rejista ya
silaha.
No comments:
Post a Comment