ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 10, 2016

NAIBU WAZIRI STELLA MANYANYA AMEMSIMAMISHA KAZI MKUU WA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII MKOANI SIMIYU.

 Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (kushoto) akitoa maelekezo kwa Kaimu Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Bi. Levina Mrema (kulia) aliyemteua wakati alipokuwa katika ziara yake ya siku moja  Mkoani Simiyu.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mhandisi Stella Manyanya amemsimamisha kazi aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Bunamhala, Bw. Ramadhani Said kilichopo Halmashauri ya Mji wa Bariadi Mkoani Simiyu, kutokana na utendaji usioridhisha na kumteua Bi. Levina Mrema kushikilia wadhifa huo.
Aliyekuwa Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii, Bunamhala Ramadhani Saidi (Aliyesimama) akitoa maelezo juu ya chuo hicho kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya (hayupo pichani) wakati wa ziara yake.

No comments: