ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 11, 2016

RC SHINYANGA AFANYA ZIARA WILAYANI KISHAPU, ATEMBELEA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI

Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakiwa wamejipanga katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa wilaya kumpokea mgeni, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tarek anayewasili kwnye gari.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Tarek amefanya ziara wilayani Kishapu na kutembelea shule mbalimbali za msingi na sekondari katika kata za Mwataga, Uchunga, Kishapu, Mwadui Lohumbo na Maganzo.

Tarek aliipongeza halmashauri ya wilaya hiyo kwa juhudi zake za kutengeza mawadati ambayo ni idadi kidogo kimebaki kabla ya kukamilisha kabisa agizo la Rais John Magufuli.

Alisema kuwa hiyo ni hatua nzuri huku akihimiza watengaji kukamilishaji mapema utengenezaji na usambazaji wa madawati katika shule ambazo bado hazijakamilishiwa zoezi hilo.
Aidha mkuu huyo wa mkoa aliwataka kuhakikisha madawati anapelekwa shule husika huku akiagiza ufanyike ukaguzi kubaini idadi kamili ya wanafunzi walioandikishwa, waliopo na watoro shule na kuchukua hatua.

Aliagiza watendaji wa kata kuwakamata wazazi wenye watoto watoro na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine wasiofuatilia mwenendo wa watoto wao shuleni.

Kwa upande mwingine aliwataka watumishi wa halmashauri hiyo kujituma na kufanya kazi kwa bidii na kuonya wavivu kwani watakwamisha maendeleo ya wananchi.

Tarek alihimiza kuwepo kwa umoja na mshikamano miongoni mwa watumishi ili kazi ziende vizuri kwani umoja ni mshikamano na kuwa watumishi wakitengana kazi itakuwa ngumu.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kishapu wakisimama kutambulishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati wakikao kifupi alipowasili wilayani humo kwa ziara.
Wakuu wa idara mbalimbali kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu wakisimama kutambulishwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga wakati wakikao kifupi alipowasili wilayani humo kwa ziara.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga akisoma taarifa za maendeleo kuhusu halmashauri hiyo wakati wakikao na mkuu wa mkoa.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mwataga Kata ya Mwataga wilayani Kishapu, Mzee Joel akimuongoza Mkuu wa mkoa na ujumbe wake walipofanya ziara shuleni hapo.

No comments: