Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Bi. Barbara Gonzalez akielezea jinsi wanafunzi hao 10 watakavyoweza kufaidika na udhamini wa Mo Dewji Foundation.
Mkurugenzi wa masomo ya shahada za awali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Allen Mushi akizungumzia mchakato wa kupata wanafunzi 10 ambao watapata udhamini wa Mo Dewji Foundation.
Mkurugenzi wa masomo ya shahada za awali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Allen Mushi na Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Bi. Barbara Gonzalez wakipongezana mara baada ya kufanya uzinduzi.
Baadhi ya watumishi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi wa mpango wa ufadhili kwa wanafunzi wa UDSM.
Na Mwandishi wetu
Mo Dewji Foundation kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – UDSM Imezindua rasmi mpango wa ufadhili kwa wanafunzi 10 wa elimu ya juu waliomaliza kidato cha sita mwaka huu wa 2016 (MO Scholar Program) kwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam leo Jumatano Septemba, 7 2016.
Mpango huu wa ufadhili kwa wanafunzi umelenga kuwawezesha wanafunzi wenye sifa tatu, wasio na uwezo wa kujilipia ada ya chuo, wanafunzi ambao wameshiriki vyema katika michezo na uongozi wakiwa shuleni na wanafunzi ambao wamefaulu kwa kiwango cha alama 1 na 2 (division 1 & 2)
Mkuu wa Taasisi ya Mo Dewji, Bi. Barbara Gonzalez amesema kuwa wameanzisha mpango huo kwa lengo la kusaidia sekta ya elimu nchini Tanzania kwa kutoa msaada wao wa udhamini wa elimu ya juu kwa wanafunzi waliomaliza kidato cha sita.
“Mpango wetu kwa muda wa miaka mitatu hadi minne ni kusaidia zaidi Tanzania lakini hapo baadae kama tukifanikisha malengo yetu Tanzania tutakwenda mbali zaidi,” ameongeza Barbara.
Aidha Mkurugenzi wa masomo ya shahada za awali katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Allen Mushi ameelezea kuwa chuo kikuu cha Dar es salaam kimelenga kusaidia wanafunzi wote wa kitanzania ambao wanasifa za uhitaji wa ufadhili na ameomba vyombo vya habari visaidie kusambaza ujumbe kwa watanzania ili wanafunzi wafaidike na mpango huo.
“Tumeanza na Chuo Kikuu cha Dar es salaam, tutaangalia namna ambavyo mpango na tutaenda na hapo baadae tutatanua mikono yetu kwenda vyuo mbalimbali,” amesema Barbara.
Na kwa mtahiniwa ambaye anakuwa anahitaji kutuma maombi kwa ajili ya kupata ufadhili wa Mo Dewji Foundation kwa ajili masomo ya chuo kikuu anaweza kuingia tovuti ya modewjifoundation.org
No comments:
Post a Comment