Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akiwa katika mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC) Jaji Slivia Fernandez de Gumendi. Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ubalozi wa Tanzania, Rais wa ICC alitumia fursa hiyo kutoa shukrani zake kwa Tanzania kwa hotuba ambayo si tu ilikuwa na ushauri wa namna ya kuimarisha ushirikiano baina ya Mahakama hiyo na Wanachama wa Mkataba wa Roma hususani kutoka nchi za Afrika lakini pia kwamba ilikuwa ni hotuba ya uwiano. Jumatatu wiki hii Tanzania ilikuwa kati ya nchi zilizozungumza wakati Ripoti ya utendaji kazi ya ICC ilipowasilishwa katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Balozi Tuvako Manongi na Rais wa ICC Jaji Gumendi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao ambayo yaligusia masuala mbalimbali kuhusu Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ( ICC)
Na Mwandishi Maalum, New York
Rais wa Mahakama ya
Kimataifa ya Makosa ya Jinai (
ICC) Jaji Slivia Fernandez de Gumendi, jana (Ijumaa), amekutana na kufanya mazungumzo na
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Matiafa, Balozi Tuvako Manongi
Katika Mazungumzo
hayo baina ya Jaji Gumendi na
Balozi Manongi yaliyofanyika katika Uwakilishi wa Kudumu wa
Tanzania, Rais wa ICC aliishukuru
Tanzania kwa hotuba yake iliyotolewa na Balozi siku ya Jumatatu wakati Baraza Kuu la Umoja
wa Mataifa, lilipopokea na kujadilia Ripoti ya ICC.
Kwa mujibu wa
Rais wa ICC Jaji Slivia Fernandez
de Gumendi hotuba ya hiyo ya
Tanzania ilikuwa yenye
uwiano (balanced) na pia
ilitoa ushauri au mapendekezo ya
namna gani Mahakama hiyo inavyoweza kuboresha uhusiano na
wanachama wake kwa mujibu wa
Mkataba wa Roma.
“
Nilikusikiliza kwa makini
sana wakati ulipokuwa unatoa hotuba yako, nilinukuu
kila hoja ulizokuwa unazizungumza . Hotuba ya Tanzania ilikuwa yenye uwiano (balanced)
na ningependa kuitumia fursa hii kuishukuru Tanzania kwa hilo.
Rais huyo wa ICC amekiri kwamba anadhani ni
wakati muafaka kwa wadau wa pande mbili
kukaa na kuzungumza kama ambayo Tanzania
na wanachama wengine wameshauri
hasa kutokana na kile alichosema, kwamba,
kila nchi imekuwa na tafsri tofauti
na uelewa tofauti kuhusu baadhi
ya vipengere (articles)
zinazohusu Mkataba wa Roma unaounda Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai.
Kwa upande wake Balozi Manongi
amesema, ushauri na mapendekezo
ambayo yametolewa na Tanzania pamoja na nchi nyingine hayalengi
katika kutaka kubadili
Mkataba wa Roma au kuipunguzia nguvu ya
kiutendaji Mahakama hiyo.
“Tungependa sana ieleweke kwamba tunaposhauri kukaa na
kuzugumza kusitafsiriwe kana kwamba
tunataka kupunguza nguvu ya utendaji wa
chombo hiki ambacho wote
tunaamini kwamba kinastahili kuwapo.
Tunashosema na kusisitiza, kwamba
kila upande unahoja za msingi basi tuzijadili kwa kuzungumza”
akasisitiza Balozi Manongi.
Rais wa ICC na
Balozi Manongi walibadilishana
mawazo juu na masuala mbalimbali kuhusu
utendaji kazi wa Mahakama ya ICC ikiwa
ni pamoja na kuangalia ni maeneo gani
ambayo Mahakama na wanachama wake
wanaweza kujadiliana .
No comments:
Post a Comment