ANGALIA LIVE NEWS

Friday, December 16, 2016

DKT. SHEIN AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA BRIGEDIA JENERALI MHAIKI, ZANZIBAR LEO

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki aliyekua Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, aliyefariki juzi katika hospitali ya Jeshi la Wananchi JWTZ Lugalo Dar es Salaam, ukibebwa na askari kupelekwa sehemu maalum kwa shughuli ya kuuagwa rasmi leo kabla kupelekwa kijijini kwao kwa mazishi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) ​akifuatana na W​aziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt.​​Hussein Ali Mwinyi (kushoto) na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) wakati Rais alipofika leo katika Hospitali ya Jeshi la Wananchi JWTZ Lugalo Dar es Salaam kwa ajili ya kuuaga mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki aliyekua Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar,aliyefariki juzi hospitalini hapo baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa ​akitoa heshima ya mwisho leo kwa mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki aliyekua Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar,aliyefariki juzi katika hospitali ya Jeshi la Wananchi JWTZ Lugalo Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa ​akitoa mkono wa pole kwa wanafamilia wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki aliyekua Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar,aliyefariki juzi katika hospitali ya Jeshi la Wananchi JWTZ Lugalo Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mfupi, ​baada ya kutoa ​heshima ya mwisho leo,kwa mwili wa ​Marehemu. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ​akitia saini kitabu cha kumbukumbu ya Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki, aliyekua Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar,ambae alifariki juzi katika hospitali ya Jeshi la Wananchi JWTZ Lugalo JIjini Dar es Salaam,baada ya kuugua kwa muda mfupi na kuagwa leo.
Jeneeza lenye Mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki aliyekua Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar,aliyefariki juzi katika hospitali ya Jeshi la Wananchi JWTZ Lugalo Dar es Salaam,ukibebwa na askari kupelekwa sehemu maalum ambapo utaagwa rasmi leo kabla kupelekwa kijijini kwao kwa mazishi.
Baadhi ya Maafisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ waliofika leo katika hafla ya kuuaga Mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki aliyekua Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar,aliyefariki juzi katika hospitali ya Jeshi la Wananchi JWTZ Lugalo, baada ya kuugua kwa muda mfupi,ambapo utaagwa leo katika Hospitali Lugalo Dar es Salaam.
Wananchi mbali mbali na jamaa waliofika leo kuuagawa Mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki aliyekua Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar,aliyefariki juzi katika hospitali ya Jeshi la Wananchi JWTZ Lugalo Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Viongozi pamoja na Wazee wa Chama leo walijumuika na Maaskari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania katika kuuaga Mwili wa Marehemu Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki aliyekua Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar,aliyefariki juzi katika hospitali ya Jeshi la Wananchi JWTZ Lugalo Dar es Salaam, baada ya kuugua kwa muda mfupi. Picha na Ikulu.

1 comment:

A.Ndomba, Washington, D.C.,USA said...

R.I.P. Brigedia Jenerali Cyril Ivor Mhaiki. Ulikuwa Rafiki mwema toka enzi za utoto wetu. Mwenyezi Mungu amekuita nyumbani. Pumzika kwa Amani Daima na Milele. I will miss you dear friend, and so is our nation and the people of Tanzania. Kwa Leticia, Charity, John na familia yote ya Mhaiki, Tafadhali muwe pole sana.