ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, December 17, 2016

DR MWELE MALECHELA AFUNGUKA ASEMA SAFARI ITASONGA KWA MSAADA WA MUNGU

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu, NIMR, Dr Mwele Malecela, ametoa kauli yake baada ya uteuzi wake kutenguliwa na Rais Dkt John Magufuli, Ijumaa hii.

Kutenguliwa kwake kumekuja siku moja tu baada ya kuzungumza na waandishi na kudai kuwepo kwa virusi vya Zika nchini. Alisema kati ya watu 533 waliopimwa wakati wa utafiti walioufanya, asilimia 15.6 waligunduliwa kuwa na virusi hivyo. Taarifa yake, ilikuja kukanushwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu.

Akijibu tweet iliyosema, ” Pole sana @mwelentuli safari yako na isonge mbele Dada,” Dr Mwele amesema, “Ahsante na itasonga kwa msaada wa Mungu.”

Tweet nyingine alijibu: Ahsante Mathew. Nilipewa dhamana nimetumikia ninamshukuru Mungu kwa nafasi ya kutumikia WaTanzania kupitia utafiti.”

7 comments:

Anonymous said...

Am I missing something here? Sijaelewa, aliye elewa naomba anieleweshe. Kutenguliwa nafasi hiyo ni kupinga research findings au?

Anonymous said...

Mwenyezi Mungu atakusaidia tu dada mwele,Mungu huwa hafungi milango yote,Mungu amekuandalia kazi nyingine nzuri sana iko njiani, anything happens is for a reason,Mungu ni mwema daima na anakupenda sana na atazidi kukupigania milele na milele

Anonymous said...

Well, wadau tunachanganyikiwa for nothing. Hajatenguliwa fani yake, kwani she is a Research Zoologist (PhD) by trade. However, ametolewa kile cheo cha UKURUGENZI. That being said, ataendelea kufanya kazi yake kama mtafiti popote pale anapotaka ulimwenguni. I don't see why people are so touched by her firing!

Anonymous said...

Ni kwakutokufuata taratibu. Whether taarifa aliyoitoa ni sahihi or not kuna taratibu zake ambazo unfortunately hakuzifuata.

Anonymous said...

Bora akafanye kazi nje ya nchi Tanzania mchosho tu hakuna mpango

Anonymous said...

Mdau hata huko nje hufanyakazi kwa kufuata taratibu.Na hakuna sehemu ambapo hakuna job security kama nje.You mess - up, you go.

Anonymous said...

Mdau hata huko nje hufanyakazi kwa kufuata taratibu.Na hakuna sehemu ambapo hakuna job security kama nje.You mess - up, you go.