ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, December 17, 2016

PICHA NA HABARI KAMILI YA AJALI YA GARI LA MHE. JOSEPH MBILINYI

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (SUGU)
Gari la Mbunge wa Mbeya mjini Mheshimiwa Joseph Mbilinyi (Sugu) Toyota Land Cruser T.161 CPP likiwa ofisi za Usalama barabarani jijini Mbeya baada ya kugonga mtembea kwa miguu na kusababisha kifo .
Na JamiiMojaBlog,Mbeya
Mkazi wa Iyunga jijini Mbeya ambaye amefahamika kwa jina moja la Rechal (13) amefariki dunia mara baada ya kugongwa na gari , namba T161 CPP Toyota LandCruiser inayodaiwa kumilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini, Joseph Mbilinyi maharufu kwa jina la (SUGU), kwenye kivuko cha barabara (ZEBRA) na kumsababishia kifo chake papo hapo.

Tukio hilo limetokea leo Desemba 17 majira ya saa mbili asubuhi huko katika eneo la Iyunga Jijini hapa, wakati gari ya Mbunge huyo ikiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege wa Songwe kwa ajili ya mapokezi ya kiongozi wa Kitaifa Freeman Mbowe.

Imeelezwa kuwa, gari hilo likiwa katika mwendokasi linadaiwa kukiuka sheria za barabarani kwa kutosimama kwenye kivuko cha barabara kinachowaruhusu watembea kwa miguu kuvuka na kumgonga mtoto huyo na kusababisha kifo chake papo hapo.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wakizungumza , kwa nyakati tofauti , wamesema mtoto huyo akiwa na mama yake walikuwa wakivuka barabara baada ya magari ya upande wa pili kusimama na kuwaruhusu watembea kwa miguu hao kuvuka.

Amesema, wakiwa katikati ya kivuko hicho mama wa marehemu alishangaa kuliona gari ya Mbunge hiyo ikija kwa kasi hivyo kumuachia mtoto wake aliyekuwa amemshika mkono na yeye kutafuta njia ya kujiokoa.

Wameeleza kuwa licha ya dereva wa gari ya Mbunge kuona madereva wenzie wa magari yaliyokuwa yakitokea Mbalizi wakisimama kwa ajili ya kuwaruhusu watembea hao kuvuka lakini yeye akitokea mjini Mbeya alishindwa kutii sheria hiyo na kupita akiwa katika mwendo kasi.

“Madereva wenzie tumesimama ili mama na mtoto wavuke lakini yeye akiwa na haraka alipita tu, kwa kweli hii inauma sana, nasikia mtoto amepoteza maisha lakini mama amejeruhiwa na kwamba amekimbizwa hospitali Teule ya Ifisi kwa matibabu,”alisema mmoja wa mashuhuda hao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari akizungumza kwa njia ya simu amekiri kutokea kwa tukio hilo na kuthibitisha kifo cha mtoto huyo.

Aidha Kivadashari ametaja jina la dereva wa gari hiyo kuwa ni Gabriel Endrew alimaarufu Dj BBG (43) mkazi wa Mwakibete jijini hapa.

Amesema hilo limetokea majira ya saa mbili asubuhi ambapo gari T161 CPP ilimgonga mtembea kwa miguu ambaye ni mtoto anayekadiriwa miaka 13 ambapo amefahamika kwa jina moja la Rechal na kumsababishia kifo wakati akikimbizwa hospitali .

Pia, aliongeza kuwa gari hiyo imekamatwa na dereva anashikiliwa na polisi kwa ajili ya mahojiano na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Mwisho.

2 comments:

Anonymous said...

Like father like son, waswahili wanasema ubora wa tunda huanzia mtini. Yeye Sugu mwenyewe hana maadili hana adabu,hana heshima sasa hao watu wake wakaribu watajifunza wapi nidhamu? Dereva wa kiongozi ni mtu anaevaa tabia za bosi wake kwa asilimia 85% . Kwanza kabisa mimi ninaimani kubwa kama ni Mbowe ndie mgeni aliekuwa akifukuziwa kwenda kupokewa na hilo gari lilomgonga na kumua huyo mtoto basi haingii akilini kabisa kama hilo gari lilikuwa haliendeshwi na yeye mwenyewe Sugu? Kuna asilimia 85% yakwamba Sugu mwenyewe ndie aliehusika na hiyo ajali ila baada ya tokeo tunaelezwa dereva na wala sio dereva wake? Kwa mambo ya kiafrika ni vitu vidogo sana kuchezwa mchezo mchafu hasa inapotokezea kiongozi fulani kuhusika na kashfa. Tusubiri na tuone nini kitafuatia baada ya kifo kilicho sababishwa na uzembe wa barabarani wakati watanzania wanawalilia wabunge wao waikomalie serikali ili kupunguza vifo vinavyosababishwa na uzembe wa madereva barabarani wabunge wenyewe ndio hao.

Anonymous said...

Asante mtoa mchango wako. Naona umekuja kwa kasi bila kutulia na kujua unachokiandika kikoje! Mwenye gari hakuwepo hakuna sababu ya kumhusisha moja kwa moja na tukio hilo wala tabia! Hizo asilimia umezifanyia utafiti gani??