Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), wakati alipotembelea ofisi hizo mkoani Mwanza.
Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), Bw. Erick Hamis akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu hali ya utendaji wa kampuni hiyo katika ukanda wa Ziwa Viktoria, mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na menejimenti na wafanyakazi wa Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), wakati wa ziara ya Waziri huyo katika ofisi hizo mkoani Mwanza.
Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza John Mongella, wakati
alipotembelea ofisi za Kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), mkoani Mwanza.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema atabadilisha
uongozi wa menejimenti ya kampuni ya Huduma za Meli Nchini (MSCL), kwa
kushindwa kutekeleza uendeshaji na usimamizi wa kampuni hiyo.
Akizungumza
na wafanyakazi wa kampuni hiyo mara baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Kaimu
Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo na kuonesha kutoridhishwa na huduma zinazotolewa na
MSCL, Prof. Mbarawa amesema kutokana na kampuni kushindwa kujiendesha kibiashara
na kulipa mishahara kwa wafanyakazi wake amelazimika kuchukua maamuzi hayo ili
kuinusuru kampuni hiyo.
“Sijaridhishwa
na taarifa za mahesabu yenu katika uendeshaji wa huduma za meli katika ukanda
wa Ziwa Viktoria, Hamuwezi kusafirisha mizigo milioni 3.6 na nyie mkapata faida
ya laki 2.. hamuomyeshi umakini kwenye utendaji”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha,
katika kuhakikisha huduma za Kampuni hiyo zinaimarika Serikali kupitia Waziri
huyo imeahidi kutoa kiasi cha shilingi
milioni 100 kwa ajili ya ukabarati wa meli nne zilizokuwa zimekufa katika
ukanda huo ili kuboresha huduma za usafiri wa Ziwa.
Prof.
Mbarawa amezitaja meli zitakazokarabatiwa ni Mv. Clarious, Mv Serengeti, Mv
Sangara na Mv. Ukerewe ambazo zinahitaji ukarabati wa injini, mifumo ya umeme
na ufundi na gia boksi.
Amewatahadharisha
watumishi wachache wanaofuja fedha katika kampuni hiyo na wale wazembe
wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao kuacha maramoja kwani Serikali haitamvumilia
mtumishi anayefanya vitendo hivyo.
Kwa
upande wake Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo, Bw. Erick Hamis, amezitaja changamoto
mbalimbali zinazoikabili MSCL, kuwa ni uhaba wa watumishi wenye weledi na
ujuzi hususan wenye taaluma ya
uhandisi na kukosekana kwa mfumo imara
na wakisasa wa udhibiti na ukusanyaji mapato.
“Kampuni
inapoteza mapato kutokana na mfumo wa kizamani wa ukusanyaji mapato, fedha
nyingi zimekuwa zikipotea na kutumika kusikojulikana, hivyo basi tumeamua
kuhakikisha tunaboresha mfumo huu ili kupata mapato zaidi”, amesema Kaimu
Meneja Mkuu.
Naye,
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella,
ameipongeza serikali kwa hatua iliyochukua ya ukarabati wa meli ya Mv Serengeti
ambayo ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Bukoba katika usafirishaji wa ndizi na
mbao.
Amewasihi
wafanyakazi kuondoa dhana iliyojengeka ya kufanya kazi kiholela na kwa mazoea
na badala kutoa ushirikiano kwa Kaimu Mkuu huyo na Menejimenti itakayoundwa ili
kufufua upya kampuni hiyo.
Imetolewa na Kitengo cha
Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
No comments:
Post a Comment