ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, December 15, 2016

MASHINDANO YA SCOUT KANDA YA AFRIKA MASHARIKI YAFANYIKA ARUSHA




Skauti wa TZ na wengine wa nchi za Afrika Mashariki wakipita
mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kambi ya mashindano ya 
skauti nchi za afrika mashariki inayoendelea mkoani Arusha 
Skauti Tz na wengine kutoka nchi za afrika mashariki 
wakimsikiliza mgeni rasmi wakati wa ufunguzi rasmi wa kambi ya 
mashindano inayoendelea mkoani Arusha
Skauti kutoka Kenya na wengine wa nchi za Afrika Mashariki 
wakipita mbele ya mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa kambi ya 
mashindano ya skauti nchi za afrika mashariki inayoendelea mkoani 
Arusha.

Na Woinde Shizza,Arusha

Vyama vya scout kanda ya Afrika Mashariki vimekutana mjini hapa kuanza mashindano ya mascout yenye lengo la kuwezesha vikosi vya scout kushindana pamoja ili kujipima katika utekelezaji wa programu ya vijana ya stadi za kiscout katika vikosi na jumuiya ya afrika mashariki ambazo
wamekuwa wakijifunza katika maeneo yao.

Akizungumza katika mashindano hayo yalioanza jana meneo ya kisongo jijini hapa,kamishna mkuu wa chama cha skauti tanzania Rashidi Mchata alisema kuwa mashindano hayo yameshirikisha vijana wa kiscout kutoka nchi tano za jumuiya ya afrika mashariki.

Mchata alisema kuwa mashindano hayo yatahusisha makundi ya mascout wadogo mascout wakubwa na masouti vijana kutoka kila nchi yatashindana kutengeneza stadi za kiskauti kwa kutumia mbinu zao ambazo wamekuwa wakifundishwa katika vikosi vyao kwa ajili ya kuwawezesha kuhudumia jamii na kuwafanya wawe wazalendo.

"Vyama vya mascout kutoka jumuiya ya afrika tumekutana hapa arusha kwa malengo matatu ikiwemo mashindano ,jukwaa la vijana mascout lakini pia tumekuwa na mkutano mkuu wa makamishna wa skauti kutoka nchi za jumuiya na hii inasaidia kwa pamoja kuhakikisha kuwa vijana wetu wanakuwa wazalendo na kupitia haya mashindano tutaweza kuwapata washindi ambao wanawakilisha nchi zao walizotokea"alisema Mchata.

Rehema Ramadhani mwanascout kutoka dar es salaam ambae anawakilishaTtanzania katika mashindano hayo alisema kuwa mashindano hayo yanajumuisha mambo yote waliokuwa wanafundishwa kuanzia ngazi ya wilaya na kwamba yanawapa uzoefu wa stadi zao kutoka kwa mascout wa nchi nyingine za jumuiya ya afrika mashariki.

Alisema kuwa katika vikosi vyao wamekuwa wakifundishwa mambo mbali mbali ikiwemo utunzaji wa mazingira kama ilivyo kauli mbiu ya rais magufuli lakini pia jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu au jamii pale inapopata janga na hivyo wanaamini kuwa wataiwakilisha tanzania kuwa mshindi katika mashindano

Kwa upande wake mwenyekiti wa jukwaa la vijana wa kiscout katika jumuiya ya afrika mashariki Murtadhwa Abdallah alisema kuwa taasisi mbali mbali zinatakiwa kujitokeza na kushirikiana katika kufadhili scout kwani vyama hivyo vimekuwa vikikabikiwa na changamoto ya fedha hivyo kushindwa kujiendesha vyenyewe.

No comments: