Profesa Yunus Mgaya ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Profesa Yunus Mgaya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).
Profesa Yunus Mgaya anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Mwele Malecela ambaye uteuzi wake umetenguliwa jana usiku kutokana na kutoa taarifa za kuwapo ugonjwa wa zika nchini.
Taarifa ya Ikulu imesema uteuzi wa Profesa Mgaya unaanza mara moja.
Profesa Mgaya alikuwa Mkugenzi Mkuu wa Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) kabla ya uteuzi wake kutenguliwa Mei mwaka huu.
Hata hivyo, baadaye Rais Magufuli alikutana naye katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kumweleza yeye ni mtu mzuri na angempa kazi nyingine.
No comments:
Post a Comment