Na Mussa Mbeho,KaTavi
BARAZA la madiwani katika halmashauri ya wilaya ya Nsimbo mkoani katavi limepitisha makisio ya bajeti yake ya maendeleo ya kiasi cha sh 24,886 ,569,000 Kwa ajili ya kufanikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ya maendeleo katika msimu mpya wa mwaka wa fedha 2017/2018.
Akifafanua bajeti hiyo Mkurugenzi mtendaji wa halmashuri hiyo Bw.Mwailwa Smith Pangani alisema halmashauri hiyo inatarajiwa kukusanya kiasi cha sh bilioni 1.5 kutokana na vyanzo vyake vya mapato ya ndani .
Alieleza kuwa kuwa fedha za ruzuku kutoka serikali kuu ni Bilioni 9.6 sawa na asilimia 39 zitatumika kulipa mishahara ya watumishi,Shilingi bilioni 2.1 sawa na asailimia 8% kwa matumizi ya kawaida huku shilingia bilioni 12.3 sawa na asilimia 50 zikitumika kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo.
‘Katika bajeti hii tumedhamiria kukamilisha miradi viporo yote, vyumba 82 vya madarasa na nyumba 17 za walimu katika shule mbalimbali za msingi na sekondari ikiwemo nyumba za waganga na maghala ya kuhifadhia mazao vitakamilishwa’, alisema PANGANI. .
Aliongeza kuwa halmashauri ya nsimbo inategemea kuendelea kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa vikundi vya vijana na wanawake wajasiriamali ili kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.
Adha Bwana Bw.Mwailwa Smith Pangani Alipongeza mchango mkubwa uliotolewa na madiwani wa halmshauri hiyo kuanzia maandalizi ya bajeti hiyo hadi kuwasilishwa kwake kwani wamesaidia sana kufafanua mikakati iliyowekwa na halmashauri kwa lengo la kuharakisha maendeleo ya wananchi.
Alisema mawazo mazuri yaliyotolewa na waheshimiwa madiwani yamesaidia katika kufanikisha utekelezaji wa shughuli zote za maendeleo katika wilaya hiyo sanjari na kuongeza ufanisi katika suala zima la ukusanyaji mapato.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mh.Raphael Kalinga pamoja na kulipongeza baraza kwa kupitisha bajeti hiyo ya mwaka wa fedha 2017/2018 amesema miradi ya maji imetengewa shilingi bilioni 4,387,999,676 ambapo kati ya kiasi hicho shilingi 4,187,999,676 zinatoka benki ya dunia na Shilingi Milioni 200 kutoka Tamisemi.
No comments:
Post a Comment