ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, January 29, 2017

TASAF YAWAINUA WANANCHI KUICHUMI

Na Mussa Mbeho ,Katavi

Mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF Mkoani katavi umesaidia kuwainua kiuchumi wanachi baada ya kuwapatia fedha na kuazisha miradi mbalimbali ya maendeleo katika kaya zao.

Wakizugumza mbele ya katibu Tawala wa mkoa wa katavi PAUL CHAGONJA baadhi ya wanufaika mradi huo Wamesema kuwa pindi wanapopatiwa fedha hizo wamekuwa wakibuni na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo kwa kiasi kikubwa umesaidia kubadilisha maisha yao .

Walisema wamekuwa wakizitumia fedha hizo kununulia mifugo kama vile kuku, bata ,ng’ombe ,mbuzi ,kondoo na Nguruwe ambazo zinawaingia kipato kikubwa baada ya kuzaliana na kusaidia kuuza na kupata mahitaji mbalimbali ya familia zao ikiwa ni pamoja na kusomesha watoto wao kutokana fedha wanazozipata kwa kuuza mifugo hiyo.

Aidha Wanufaika hao wameiomba serikali kuendelea kutoa fedha hizo ili kuweza kuwasaidia watanzania wengine wasiokuwa na uwezo zaidi kuendelea kunufaika na mradi huo .

Nae Afisa maendeleo ya jamii mkoa wa katavi bwana Iginas Kikwala Alisema mko wa katavi umeanza kutoa fedha za mradi huo wa Tasaf kwa awamu ya kumi na tano kuanzia jana katika wilaya zote kwa utaratibu mpya wa walengwa kufika wenyewe katika vituo vya kuchukulia fedha ili kuweza kuondokana na malalamiko kwa baadhi yao.

Kikwala Alisema kuwa jumla ya shilingi billioni 257,251,475 zinatarajiwa kugawiwa kwa walengwa wa mradi huo katika mkoa wa katavi huku akiwataka wanufaika kuendelea kubuni na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuweza kuondokana na umasikini katika kaya zao.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa mkoa wa Katavi PAULO CHAGOJA Amewapongeza wanufaika wa mradi huo mkoani hapa kwa kuzitumia vizuri fedha hizo wanazopewa na Tasaf katika kubuni na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo kwani fedha hizo zietolewa na wafadhili kutoka nchi mbalimbali ili ziweze kusaidia wananchi kuondokana na umasikini

Hata hivyo CHAGONJA Ametoa wito kwa viongozi wote wa serikali wanaohusika katika kusimamia zoezi la ugawaji wa fedha za mradi huo mkoani hapa kutenda haki kwa kuwapatia walengwa na kuongeza kuwa atakae bainika kufanya ubadhilifu katika fedha hizo sheria kali itachukuliwa dhidi yake .

No comments: