Kesi inayowakabili wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee wa Kawe, Mwita Waitara wa Segerea na Saed Kubenea wa Ubungo, ya kudaiwa kumfanyia shambulio la kudhuru mwili Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresia Mmbando, leo imeshindwa kusikilizwa baada ya hakimu aliyetakiwa kuisikiliza kuwa likizo.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka iliyofunguliwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu, inadaiwa kuwa wabunge hao pamoja na makada kadhaa wa Chadema, walifanya tukio hilo Februari 27, mwaka jana wakati Mmbando akisimamia mkutano wa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.
Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Februari 13, mwaka huu ambapo mwandishi wetu aliwashuhudia Mdee na Waitara wakitoka kwenye viunga vya mahakama hiyo, asubuhi ya leo.
Awali, kesi hiyo ilikuwa ikisikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu, Huruma Shaidi, Wakili wa Utetezi, Fredrick Kihwelo huku wakili wa serikali akiwa ni Diana Lukundo.
No comments:
Post a Comment