Nadhiri hiyo imetokana na ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) katika miradi kadha ya Manispaa ya Dodoma ukiwemo wa Chigongwe ambao ulionekana kujawa na madudu kibao.
Selasini amesema, mazingira yaliyopo katika mradi huo yanapingana na kauli ya Kaimu Mhandisi wa Maji wa Manispaa ya Dodoma, Majuto Eliufoo ambaye aliomba kamati hiyo kumpa wiki mbili ili maji yaanze kutoka.
Mbunge huyo pamoja na kusema hayo, pia aliungana na wabunge na Mkurugenzi wa Manispaa ambao wamesema wazi kwamba haiwezekani katika wiki mbili maji yatoke na yeye (Eliufoo) kung`ang`ania kuwa itawezekana.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, tuwe wakweli kwenye mambo ya msingi, na mimi nataka kuweka ukweli kwenye kumbukumbu kwamba, mradi huu ukianza kufanya kazi ndani ya wiki tatu tangu leo lazima na nisisitize kuwa itakuwa lazima kwa mimi kujiuzulu nafasi yangu ya ubunge,” amesema Selasini.
Mbunge huyo amesema anazo taarifa kuwa mradi huo wa maji katika eneo hilo ulianzishwa kisiasa ndiyo maana wataalamu hawajui chochote.
Mhandisi Eliufoo amesema, mradi huo una thamani ya Sh milioni 533 na tayari mkandarasi Kampuni ya Buyungu General Enterprises imeshalipwa kiasi cha Sh milioni 409 huku akisema kazi katika mradi imemalizika kwa asilimia 95.
HABARI LEO
No comments:
Post a Comment