ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 14, 2017

MASAUNI AWATAKA MAAFISA MAGEREZA KUONGEZA KASI YA UZALISHAJI NCHINI, AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA VITUO VYA MAGEREZA TANZANIA BARA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (mbele), kuingia ukumbini kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa Maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao.  (Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya Magereza yote Tanzania Bara (hawapo pichani) katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa  Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao
 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa akitoa hotuba yake ya kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) kwa ajili ya kuja kuufungua Mkutano wa Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara ambao pia ulihudhuriwa na Maafisa Waandamizi wa Jeshi hilo kutoka Makao Makuu, ulifanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Hata hivyo, Dkt Malewa katika hotuba yake alimshukuru Rais John Magufuli kwa kutatua kwa kiasi kikubwa changamoto ya uhaba wa nyumba za Makazi ya Askari wa Jeshi hilo pamoja na juhudi za Serikali yake za ununuzi wa  magari 450 kwa awamu ya kwanza ambapo jeshi hilo linatarajia kuyapata. Katikati ni Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza naWakuu wa Vituo vya Magereza yote Tanzania Bara katika Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa  Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano huo, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo, kuongeza kasi zaidi ya kuzalisha katika kilimo, miradi ya ufugaji pamoja na vyanzo vingine ili kulilitea mapato zaidi Jeshi hilo. Aidha, alisema kwa maafisa watakaozembea katika uzalishaji wataondolewa katika nyadhifa zao.  
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia waliokaa), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (wapili kushoto waliokaa), Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi hilo, Gaston Sanga (kulia waliokaa), Naibu Kamishna wa Jeshi hilo, Edith Mallya (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa wa Jeshi hilo, mara baada ya Naibu Waziri huyo, kuufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Makao Makuu ya Jeshi hilo pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam.

Suleiman Msuya

NAIBU Waziriwa Mambo ya Ndani, MhandisiHamadYusuphMasauniamesemaSerikalihaitasitakuchukuahatuakwawakuuwamagerezanchiniambaowatashindwakutimizadhanayauzalishajimaliambayoniagizo la Rais John Magufuli.

Aidha, Jeshi la Magereza Tanzania limetajachangamototanokuuambazozinakabilijeshihilohaliambayoinakwamishaufanisikatikamipangoyao.

Masuanialisemahayowakatiakizungumzakatikamkutanowawakuuwavituovyamagereza Tanzania Bara unaofanyikakatikaBwalo la MagerezaUkongajijini Dar es Salaam.

NaibuWazirialisemaiwapowakuuwamagerezawatatumiawafungwawaliopouzalishajiutaongezekahivyokuondokananatabiayakulalamikaufinyuwabajeti.

Alisemapamojanavigezombalimbalivyakupimawakuuwamagerezakigezokinginekitakuwanikuangaliakasiyauzalishajikwaeneohusika.

Masauni alisema jeshi la magereza lina rasilimali nyingi kama mashamba na viwanda hivyo wanapaswa kutumia fursa iliyopo kuongeza uzalishaji na kuchochea uchumi wa viwanda.

“Napenda kuwa muwazi hatutavumilia mkuu yeyote wa gereza ambaye atashindwa kuzalisha na kuendeleza fursa ambazo zinamzunguka kwani Tanzania ya viwanda itafanikiwa kupitia vyombo vilivyopo katika wizara yetu,” alisema.

Naibu waziri alisema anaamini kupitia jeshi hilo ajiraz itaongezeka, uchumi utakuwa na maendeleo ya nchi yatapatikana kwa haraka hivyo lengo la 2025 kukamilika.

Kwa upande wake Kamishna Jenerali Magereza, Dk. Juma Malewa alisema jeshi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali kama ufinyu wabajeti, madeni ya watumishi, makaziduni, ukosefu wa posho na vitendea kazi kama usafiri.

Alisema katika kutatua changamoto ta usafiri wanatarajia kupokea magari 450 siku za karibuni katiya 905 ambayo wameahidiwa na Serikali hali ambayo itaweza kutatua changamoto hiyo.

Dk. Malelwa alisema pia wameanza kutatua changamoto ya makazi ambapo Rais Magufuli ametoa sh. bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 320 katikakambiyaUkonga.

Kamishna Jenerali Malelwa alisema hadi sasa wamepokea sh. bilioni 5 ambazo zimeanza kutumika kujenga nyumba hizo 320 zinazojengwanaWakalawaMajengonchini(TBA).

Alisema wao wamejipanga kuhakikisha kuwa Tanzania ya viwanda inapatikana kwa kushirikiana na wadau mbalimbali hivyo utatuzi wa changamoto hizo utakuwa suluhu sahihi kwao.

“Tumedhamiria kuongeza uzalishaji na kufufua viwanda mbalimbali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali lakini tunaomba changamoto nilizo zitaja zitatuliwe kwa wakati,” alisema.

Akizungumzia dhana hiyo ya viwanda Mkurugenzi waViwanda, Naibu Kamishna wa Magereza Edith Mallya alisema utekelezaji wa agizo la Serikali umeanza katika baadhi ya viwanda kama MbigiriMorogoro na Karanga.

No comments: