ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 13, 2017

Maskini Jokate; Sasa Moyo Wako Usukume Damu

Na SIFAEL PAUL| IJUMAA WIKIENDA| MAKALA
PENZI ni kitendo, kitendo cha kumjali, kumfariji na kumfikiria mwenzi wako. Kuwa mwaminifu, mpole, muungwana, mwenye subira na kuelewa kuwa huyo mpenzi wako ana uhuru wa kuweza kuchagua kukupenda au kutokukupenda milele bila kuangalia hasara zitakazopatikana. Ifahamike kuwa hisia za penzi ni hisia tu, zinaweza kuja kwa wingi au kutoweka kabisa.
Endapo utaona hisia za penzi zimeanza kutoweka, unaweza kufanya jitihada kuzirudisha kwa kufanya matendo ya upendo bila kujali faida au hasara zitakazotokea, unachohitaji hapa ni kurudisha penzi lako katika mstari ulionyooka kama kweli lipo! Katika harakati za kudumisha penzi au uhusiano na mwenzi wako, inategemea na uamuzi wako wewe mwenyewe, uwe mwanamke au mwanaume.

Kwa mwanamke unapaswa kuonesha upendo zaidi kuliko kupokea, isipokuwa pale ambapo mwanaume ameshindwa kabisa kupokea upendo wako, huna namna, inakupasa kutafuta sehemu sahihi ya kutuliza mtima wako. Hicho ndicho kinachotokea kwa mwanadada Jokate Mwegelo almaarufu Kidoti au Jojo.
Msomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), mahali ambapo hapana shaka kuwa vijana wanapikwa vizuri na kutoka wakiwa ‘wamekwiva’ kupambana na maisha kwa kujiajiri au kuajiriwa.
Ukweli ni kwamba Jokate ni mrembo mwenye pilika nyingi kiasi kwamba wakati mwingine baadhi ya mashabiki wake humshangaa kwamba anawezaje kumudu majukumu yote hayo. Jokate anajihusisha na muziki, uigizaji, umodo, ubunifu wa mavazi, utangazaji, ujasiriamali au biashara, ushereheshaji, utangazaji na siasa (ni kada kindakindaki wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Lakini pamoja na harakati zote hizo na kuwa role model wa wasichana wengi (hilo sina shaka nalo), Jokate amejikuta akiingia kwenye maumivu makali ya kimapenzi ya mara kwa mara. Maskini Jokate! Ukiacha huko nyuma, Jokate aliwahi kuripotiwa kutoka kimapenzi na staa wa mpira wa kikapu Marekani, Hasheem Thabeet Manka.
Kwenye penzi hilo, Jokate alikiri mbele ya kamera ndani ya chumba chetu cha habari kuwa alikufa na kuoza kwa jamaa huyo kiasi kwamba alipomwagana naye alinusurika kujitoa uhai. Baada ya hapo, mrembo huyo alitua kwenye ‘mikono isiyokuwa salama’ ya staa wa Afro-Pop.
Nasibu Abdul ‘Diamond Sasa moyo wako usukume damu! Platnumz’, jamaa aliyesifika kucheza na hisia na mioyo ya warembo mastaa.
Penzi hilo lilipata ushabiki mkubwa kwa sababu ya mwigizaji mwenzake, Wema Isaac Sepetu aliyekuwa ametoka na Diamond. Kutoka kwa Diamond, Jokate alijikuta akiangukia kwenye penzi la hasimu wa Diamond kimuziki, Ali Saleh Kiba.
Penzi hilo lilikuwa na sarakasi kibao za kupanda na kushuka. Mara kadhaa Magazeti Pendwa ya Global Publishers ambayo huwa hayabahatishi katika kuripoti habari zake yaliripoti kuwa kulikuwa na ugumu wa kufikia kwenye ndoa kwa sababu kulikuwa na tofauti za kifamilia.
Mwangwi wa sauti ulisikika kuwa Jokate alikataliwa na wazazi wa Kiba lakini pia Kiba naye alikataliwa upande wa Jokate. Zilitajwa sababu nyingi ikiwemo ya kidini.
Jokate (Mkristo), Kiba (Muislam) Pamoja na hayo lakini pia Kiba hakupenda kuweka bayana penzi lake na Jokate badala yake Jokate ndiye aliyekuwa akikiri kwenye vyombo vya habari.
Hivi karibuni familia ya Kiba ilifanya tukio la aina yake pale ilipomkana rasmi Jokate kupitia kwa mama yao ambaye alisema hamtambui mrembo huyo kama ni rafiki wa Kiba badala yake anachojua ni rafiki wa dada wa Kiba, Zabib Kiba.
Kilichofuata ni taarifa kuwa, sasa Kiba anamuoa mchumba wake wa kitambo, Amina, mtoto wa Gavana wa Mombasa, Kenya.
Kufuatia ishu hiyo, Jokate alinukuliwa akisema kuwa, huenda familia ya Kiba haikuwa serious au walighafilika kumkana lakini akabainisha kuwa sasa yupo single (hana mpenzi). Hapo ndipo mjadala ukanoga yalipaswa kuwa kwenye levo za warembo wengine kama yeye, Nancy Sumary (mke wa Luca wa Bongo5), Jacqueline Mengi (mke wa Mengi) na Faraja Kotta (mke wa Lazaro Nyalandu).
Mwisho Jokate anapaswa kujua kuwa, hisia za kimapenzi hutokea ndani kabisa ya moyo. Kila mmoja ana uhuru na haki ya kupenda. Huwezi kuchaguliwa wa kumpenda! Mapenzi ni maisha ya mtu katika uhalisia wake hivyo Jokate kazi ni kwako! huku Jokate akiambiwa moyo wake kwa sasa usukume damu na si vingine.
Wapo wanaosema Jokate anapaswa kuwa makini endapo anataka kuingia tena kwenye uhusiano na staa au mtu maarufu. Jojo anapaswa kujua kuwa haya yanayomtokea kwenye uhusiano wa kimapenzi si mapya kwani yalishawatokea wengine hivyo yeye siyo wa kwanza duniani. Wapo wanaoamini kuwa kama kweli Jokate anataka penzi imara, basi aachane na mapenzi ya mastaa lakini wapo wachache wanaomshauri kwamba kama anaweza kukomaa na mastaa aendelee.
Hao wanatumia mfano wa Beyonce na Jay Z, Will Smith na Jada Pinket Smith ambao wote ni mastaa na wamedumu kwenye mapenzi yao. Wapo pia wanaoamini kuwa maisha ya Jokate

No comments: