Advertisements

Monday, June 19, 2017

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AFUTARISHA NA KUTOA VYETI VYA SHUKRANI KWA WADAU WA MAZINGIRA

Viongozi na Waumini ya Dini ya Kiislam mkoa wa Dar es Salaam wakiwa kwenye sala ya magharibi wakati Iftar maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Raia wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wakisoma Qasida kwenye Iftar maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti cha shukrani Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Bw. Ruge Mutahaba kwa ushiriki na ufanikishaji wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa ilifanyika Butiama.

Wengine waliopokea vyeti hivyo ni TBC, Lake Gas, TBL, WWF na ZANTAS.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkabidhi cheti cha shukrani Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Bia Tanzania TBL,Roberto Jarrin kwa ushiriki na ufanikishaji wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira Duniani ambayo kitaifa ilifanyika Butiama.

Wengine waliopokea vyeti hivyo ni TBC, Lake Gas, Clouds Media, WWF na ZANTAS.
Ndugu, Jamaa, Marafiki na Wadau kutoka sekta mbali mbali wakipata futari kwenye Iftar maalum iliyoandaliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam.

No comments: