ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 21, 2017

UPATIKANAJI WA DAWA KWENYE VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA WAFIKIA ASILIMIA 80

Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga(CMO), Jairy Khanga akifungua mafunzo ya mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha wauguzi kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga uliofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri mjini Tanga kulia ni Msimamizi wa Mfuko huo,Dina Mlwilo kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkinga 
Msimamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo akizungumza na waandishi wa habari Jijini Tanga wakati wa mafunzo ya mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha wauguzi kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga uliofanyika mjini hapa ambapo
alisema asilimia 70 wakina mama wajawazito wamejiunga na mradi wa tumaini la mama kwa ajili ya kupata matibabu 
Mwezeshaji wa mafunzo wa Tumaini la Mama,Ally Omari akisisitiza jambo wakati akitoa somo kwenye mafunzo hayo
Mmoja wa wasimamizi wa mradi wa Tumaini la Mama Tanzania Irine Meaki akielezea masuala mbalimbali wakati wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Jiji. 
Baadhi ya wauguzi wanaohudumia wakina anama wajawazito wakimsikiliza mgeni rasmi wakati alipofungua mafunzo ya mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo wakati wa mafunzo ya mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia mafunzo wakati wa mafunzo ya mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga.
Msimamizi wa Mfuko huo,Dina Mlwilo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo hayo 

UPATIKANAJI wa dawa kwenye vituo vya Afya kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga umeelezwa kufikia asilimia 80 kwa wagonjwa wanao kwenda kupata matibabu wakiwemo wanaohudumiwa na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

Hayo yalibainishwa na Mganga Mkuu wa Jiji la Tanga(CMO), Jairy Khanga wakati alipofungua mafunzo ya mradi wa tumaini la mama uliyowahusisha wauguzi wanaohudumia wakina mama wajawazito kutoka halmashauri za Tanga Jiji na Mkinga chini ya usimamizi wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga.

Alisema upatikanaji huo wa dawa umesaidia kuweza kuwadumia wakina mama wajawazito ambao wamekuwa wakijitokeza kupata huduma za matibabu na vifaa tiba pamoja na wategemezi wao.

Aidha alisema jambo hilo limeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza na kuondokana na vifo vya wakina mama wajawazito ambavyo vilikuwa vikijitokeze kutokana na kukosa huduma muhimu za matibabu wakati wanapojifungua.

Alisema kutokana na umuhimu wa mradi huo watoa huduma wanapaswa kuweka mipango mizuri ya kuwahudumia wakina mama wajawazito wakati wanapofika kwenye vituo vyao vya afya ili waweze kuepukana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na hali walizokuwa nazo.

“Mradi huu una zaidi ya miaka minne nyie kama watoa huduma mnauzoefu mkubwa hivyo kupitia mafunzo hayo jaribuni kushirikiana na wawezeshaji kuhusu changamoto zinazowakabili wakati wa utekelezaji wake “Alisema.

Aidha pia aliwataka watoa huduma wafanye uhamasishaji mkubwa kwa wakina mama wajawazito waliopo kwenye maeneo yao kwa lengo la kuongeza wigo mpana wa kuwaandikisha kwenye mradi huo ambao ni muhimu kwao.

Akichangia wakati wa uwasilishwaji wa mada mbalimbali katika mafunzo hayo,Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) wilayani Mkinga Elizaberth Dickson alisema moja kati ya changamoto kubwa zilizopo hivi sasa ni ucheleweshwaji wa kadi za bima ya afya kwa wakina mama wajawazito jambo ambalo linakwamisha huduma kwa baadhi yao wanapohitaji
matibabu.

“Lakini nisema upatikanaji wa kadi za mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa wakina mama wajawazito na wategemezi kwa wakati zitarahisisha upatinaji wa huduma za matibabu katika vituo mbalimbali vya afya ndani na nje ya mkoa”Alisema

Katika kuhakikisha huduma hiyo inawafikia wakina mama wengi mkoani Tanga, Msimamizi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Dinna Mlwilo aliwataka watoa huduma kuihamasisha jamii kuona umuhimu wa kuajiandikisha katika vituo vya afya wakati wa ujauzito kupitia mradi huo

“Kwani kujiandikisha huko wanaweza kupata fursa muhimu ya kupitia mradi wa tumaini la mama kwa kupata huduma za matibabu wao na wategemezi wao kwenye vituo vya afya “Alisema.

Aidha alisema kwa mkoa wa Tanga tayari wamekwisha kuandikisha wakina mama wajawazito asilimia 70 ambao wananufaika kupitia mpango huo ambao una lengo la kupambana na vifo wakati wanapojifungua.

Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

No comments: