Advertisements

Tuesday, July 25, 2017

MADUKA YA NGUO YA WOOLWORTHS YAJA NA PUNGUZO LA HADI 50%

Maduka ya nguo ya Woolworths yenye matawi yake jijini Dar es Salaam na Arusha, yametangaza punguzo kubwa la bei kwa bidhaa tofauti tofauti zinazopatikana katika maduka yake. Mkurugenzi wa fedha wa Woolworths Tanzania Samson Katemi alisema punguzo hilo kubwa la bei ni la hadi kufikia asilimia hamsini na litadumu kwa wiki moja kuanzia leo Jumanne. “Lengo la Woolworths ni kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anaweza kumudu kununua nguo mpya na za kisasa kwa gharama nafuu na kuachana na mitumba na ndiyo maana huwa tunakuwa na punguzo la bei mara kwa mara,” alisema.
Mkurugenzi wa fedha wa maduka ya nguo ya Woolorths Samson Katemi, akimkabidhi mshindi wa hivi karibuni wa droo ya mwezi Lilian William Divas vocha za manunuzi zenye thamani ya shilingi laki tano. Wateja wa Woolworths wanaofanya manunuzi kupitia kadi maalum za manunuzi (Wrewards) wanayo nafasi ya kujishindia vocha hizo.

Katemi alisema punguzo hili litawawezesha wateja wa Woolworths watakafanya manunuzi katika maduka yake yaliyopo PPF Towers na Mikocheni kwa jijini Dar es Salaam pamoja na TFA na Njiro Complex kwa jijini Arusha wataweza kupata punguzo hilo katika bidhaa kama nguo za watoto, wanawake na wanaume “Kwa wateja wenye kadi maalum za manunuzi za Wrewards, watapata asilimia 10 zaidi ya punguzo. Kama mteja hana kadi ya Wrewards afike katika maduka yetu ili aweze kuipata bila malipo na aweze kunufaika na asilimia10 zaidi,” alieleza
Baadhi ya bidhaa mpya zilizopo katika maduka ya Woolworths kama ambavyo kamera yetu ilifanikiwa kuzinasa katika moja ya maduka ya Woolworths yaliyopo jijini Dar es Salaam.

Katemi aliongeza kuwa, wateja wanaofanya manunuzi kwa kutumia kadi za Wrewards wanayo nafasi yakuingia kwenye droo zinazofanyika kila mwezi na kujishindia vocha za manunuzi zenye thamani ya shilingi laki tano ambazo huweza kutumika ndani ya kipindi cha miezi sita. “Katika droo ya mwezi Aprili, Lilian William Divas aliweza kuibuka mshindi. Kila mteja anayetumia Wrewards kadi kufanya manunuzi anaweza kuwa mshindi kama alivyokuwa Lilian,” aliongeza . Na katika droo ya mwezi wa sita Amina Shaban na Abdul Karim Ngarama waliibuka washindi. 
Baadhi ya wateja wakihudumiwa mara baada ya kufanya manunuzi kama ambavyo kamera ilivyokamata katika dula la Woolworths lililopo katika jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam. 
Picha juu na chini ni baadhi ya wateja wakichagua nguo mara baada ya dula la Woolworths kutangaza punguzo la bei la hadi asilimia 50 kwa bidhaa tofauti tofauti kama ambavyo kamera yetu iliwakuta katika dula la lililopo katika jengo la PPF Tower jijini Dar es Salaam.

No comments: