ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 24, 2017

Mchungaji, waumini wafikishana polisi

Ibada katika Kanisa la Anglikana lililopo eneo la Mji Mwema mkoani Mwanza, jana ilishindwa kufanyika baada ya waumini na Mchungaji wa kanisa hilo, Belnago Madams kutofautiana hadi kufikishana polisi.
Hatua hiyo ilikuja kwa kile kilichodaiwa kuwa waumini walikasirika baada ya mchungaji huyo, kuomba kuwekwa rumande kwa saa kadhaa mzee wa kanisa hilo akimtuhumu kwa kulifunga.
Wakizungumza nje ya Kituo Kikuu cha Polisi Mwanza jana, baadhi ya waumini walisema hawamtaki mchungaji huyo kutokana na matendo yake ya kujichukulia uamuzi binafsi.
Walisema siku ya tukio juzi, Mchungaji Madams alitoa taarifa kwa polisi kuwa kanisani hapo kuna vurugu, na polisi walifika lakini hawakukuta vurugu za aina yoyote kama ilivyotaarifiwa.
Wakaamua kuwapeleka kituoni mchungaji Madams, katibu wa kanisa, Anthony Lupepo na waumini wengine sita ili wakatoe maelezo.
Kwa mujibu wa mzee huyo anayejulikana kwa jina la James maregesi, walipofika kituoni saa mbili asubuhi Mkuu wa kituo (OCD) aliwataka wamsubiri mpaka atakaporejea kwasababu anatoka nje ya ofsi ana wageni. Hata hivyo, jitihada za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi hazikufanikiwa, kila alipopigiwa simu ilipokewa na msaidizi wake aliyesema yupo kwenye kikao cha ndani na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Saimon Sirro.
Kadhalika, alipopigiwa simu Mchungaji Madams na Mwandishi ambaye alijitambulisha, alimjibu kwa ukali kuwa; “sitaki upuuzi wewe achana na mimi,” huku akiiacha simu hewani bila kuikata akiendelea kufoka.
Katika maelezo yao, waumini hao akiwamo Philbert Ezekiel, alisema walipokuwa nje ya kanisa kabla ya polisi kufika, lilifika gari la Askofu wa Anglikana Dayosis ya Nyanza (DVN), Boniphace Kwangu, lakini hakushuka na baadaye aliondoka. Alipopigiwa simu ili azungumzie sakata hilo, iliita bila majibu. Hata hivyo, askofu huyo alishawahi kupigiwa simu mara mbili alijibu kuwa hawezi kuzungumza na mwandishi wa habari, ni kupoteza muda. Mwezi uliopita, waumini wa kanisa hilo wakiongozwa na walei, walitoa tamko la kumkataa askofu huyo kwa madai analigawa kanisa na walimtuhumu kufanya ubadhirifu wa mali za kanisa.
“hatumtki mchungaji huyu mana anafanya mamba yake binafsi anashindwa kuzingatia taratibu hawezi kuweka waumini ndani bila sababu yoyote” alisema muumini Stephania Rulomba
Mpaka sasa Ocd hajarudi mchungaji wa kanisa na katibu Wake wapo kaunta polisi na waumini kadhaa wapo nje ya geiti la polisi Central wakisubiria maelezo ya OCD.

No comments: